BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI AKUTWA NA SILAHA MBILI NA LUNDO LA RISASI 519 KINYUME CHA SHERIA VISIWANI ZANZIBAR.



Shotgun
http://www.zanzibardaima.net/wp-content/uploads/2013/08/Mansour-Yussuf-Himid.jpg 
Mansoor Yussuf Himid

Jeshi la Polisi Zanzibar linamshikilia aliyewahi kuwa waziri katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansoor Yussuf Himid kwa tuhuma za kumiliki silaha mbili na kiwango kikubwa cha risasi kinyume na sheria.


Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Salum Msangi alisema Himid alikutwa akimiliki risasi 519.

Pia alikutwa na silaha mbili, moja aina ya shotgun 20 BRE Na. 1904136413 ikiwa na risasi 112 na bastola 7.65 Na. F 76172W ikiwa na risasi 295.

Himid ambaye pia ni shemeji yake Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, alikamatwa nyumbani kwake Chukwani, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Msangi alisema alikutwa na silaha hizo ambazo hata hivyo kwa mujibu wa nyaraka alizonazo anazimiliki kihalali.

Alisema uchunguzi unaendelea kufanywa kuhusu kiwango cha risasi alizokutwa nazo.
“Kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar ya umiliki wa silaha mtu anatakiwa kumiliki risasi 50 tu kwa silaha ya shotgun na risasi 25 kwa bastola,” alisema Msangi.

Alisema licha ya kukiuka kanuni ya kuwa na risasi kwa upande wa Zanzibar, pia amekiuka Sheria ya umiliki wa risasi ya Tanzania inayotaka mtu kumiliki risasi 200 kwa silaha ya shotgun.

“Tunaendelea kuchunguza kwa sababu pamoja na kujua matummizi ya silaha hizi kwa mtu kujilinda, kuwinda wanyama lakini pia inawezekana mtu akazitumia vibaya,” alisema.

Alisema jeshi hilo linaweza kumuachia huru mtuhumiwa huyo mara baada ya upelelezi kukamilika huku akiwataka viongozi wafuate sheria za umiliki wa silaha.

Himid aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali SMZ na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mpaka mwaka 2013 alipovuliwa uanachama kwa tuhuma za kwenda kinyume na sera za chama hicho.

Alitangaza hadharani kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF) na nia ya kugombea uwakilishi katika Jimbo la Kiembe samaki kwa tiketi ya CUF na kuahidi atotoa nguvu za ziada ili kuhakikisha, Maalim Seif Sharif Hamad anapata urais wa zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: