MAJAMBAZI WAMPORA MSALABA NA PETE KADINALI WA KANISA KATOLIKI.
Watu waliokuwa wamejihami wamemuibia Askofu mkuu wa Rio de Janeiro nchini Brazil msalaba wake na pete
Kadinali, Dom Orani Tempesta, alikuwa njiani kuelekea kuhudhuria mkutano mjini alipovamiwa na majambazi hao.
Mmoja wa majambazi aliyekuwa na bunduki katika kanisa, alimfahamu kadinali huyo na kumuomba msamaha.
Hata hivyo, hilo halikushutua genge hilo ambalo liliendleea kumpora kadinali huyo, na hata nusura wampore gari lake.
Vitu vilivyoibwa vilipatikana baadaye.
Hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyiika Jumatatu jioni katika mtaa wa Santa Teresa.
Mwandishi wa BBC Gary Duffy, anasema kuwa visa vya wizi hutokea mara kwa mara katika mtaa huo wenye shughuli nyingi za kitalii na kwamba visa hivyo vimekuwa vikiongezeka sana mwaka huu.
Mwanafunzi wa dini pamoja na mpiga picha mmoja waliokuwa kwenye gari na kadinali huyo pia waliporwa.
Licha ya tukio hilo, kadinali aliendelea na shughuli zake huku mwanafunzi na mpiga picha wakienda kuripoti kwa polisi.
Pete ya kadinali na msalaba, vilipatikana pamoja na simu yake ya mkononi
Hata hivyo, vifaa vya mpiga picha havijapatikana.
Dom Orani Tempesta alitawazwa kama kadinali na Papa Francis mapema mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment