NDEGE KUBWA YA KISASA YA DREAMLINER YATUA UWANJWA WA GLASGOW KWA DHARURA NCHINI SCOTLAND.
Dege la kisasa Dreamliner lot aina ya boing.
Ndege kubwa na ya kisasa maarufu kama Dreamliner ikiwa na abiria 260 imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Glasgow, nchini Scotland.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Polish airline Lot ,ilikua inafanya safari yake kutoka Chicago kuelekea Warsaw ilipotangaza dharura kuwa katika hali ya dharura.
Na mara baada ya kutua abiria waliondolewa uwanjani hapo, na ndege kufanyiwa uchunguzi wa kilichosababisha itue kwa dharura ingawa mpaka sasa chanzo cha dharura hiyo hakijajulikana.
Nao uwanja wa ndege wa Glasgow uliendelea na shughuli zake kama kawaida na ndege hiyo haikuleta usumbufu wowote.
Ingawa taarifa za awali zinaonyesha kuwa ndani ya ndege hiyo kulikua na harufu ya moshi, na baadaye uchunguzi ulipofanywa ulionyesha kua hakukuwa na chanzo cha moto kilichosababisha harufu hiyo ya moshi.
0 comments:
Post a Comment