BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA RAIS KIKWETE YAKABWA KOO NA KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC), YAPEWA SIKU 30 KULIPA DENI LA SH TRILIONI 8.4.


SIKU moja baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuibana Serikali, ilipe deni la muda mrefu la Sh trilioni 8.4 kwa mashirika ya hifadhi ya jamii.

 
Pia kamati hiyo imetoa mwezi mmoja kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kuhakikisha imekabidhi ripoti yake ya ukaguzi wa msamaha wa kodi inayotolewa na Serikali.

Hatua hiyo inafuatia agizo la awali lililotolewa na kamati hiyo miaka kadhaa iliyopita na ambalo halijatekelezwa. Katika mwaka wa fedha 2012/13 misamaha ya kodi ilifikia Sh trilioni 1.5.

Hayo yalibainishwa na Naibu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Athumani Selemani, wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi wa ofisi ya CAG wa hesabu za Serikali kwa upande wa hazina za mwaka huo wa fedha 2012/13.

Pamoja na mambo mengine alisema kwa mwaka huo wa fedha, ofisi hiyo ya CAG ililazimika kuipatia hati chafu Serikali katika hesabu zake baada ya kubainika kuwa hazikuzingatia viwango vya kimataifa ambapo baadhi ya hesabu hazikujumuishwa.

“Tunafahamu kuwa hesabu hizo hazijajumuishwa kutokana utofauti wa ufungaji wa hesabu kwa mwaka wa mashirika haya ya umma, ambapo yapo mashirika yanayofunga hesabu zake mwezi Juni na mengine Desemba hali inayoleta mkanganyiko,” alisema Selemani.

Alisema tayari wameshaagiza Serikali kuliangalia suala hilo na kuweka mfumo mmoja wa ufungaji wa hesabu za mashirika ya umma utakaowezesha hesabu hizo kupatikana kwa wakati na kujumuishwa katika ripoti za hesabu za Serikali.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya PAC, Kabwe Zitto, aliitaka ofisi hiyo ya CAG, kuwasilisha ripoti yake ya ukaguzi wa misamaha ya kodi inayotolewa nchini na kutoa muda wa mwezi mmoja kazi hiyo iwe imekamilika.

Akizungumzia suala la kodi Selemani, alikiri kuwa tayari ofisi yake imekamilisha ukaguzi wa misamaha hiyo ya kodi, lakini kutokana na wingi wa taarifa na nyaraka, aliomba muda ili waweze kukamilisha kuandaa ripoti hiyo na kuikabidhi kwa kamati.

Katika ripoti hiyo ya CAG, ilibaini masuala mbalimbali ikiwemo, kuwepo kwa bohari za forodha 27 zinazofanyakazi bila kuwa na leseni halali huku kukiwa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Aidha, alisema ripoti hiyo ilibainisha tatizo la Serikali kuchelewa kutoa fedha za miradi ya maendeleo au kutokutoa kabisa ambapo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 jumla ya Sh bilioni 863 sawa na asilimia sita ya bajeti nzima hazikutolewa katika miradi hiyo ya maendeleo.

Kuhusu eneo la ukaguzi wa mashirika ya umma, alisema tayari vyama 12 vya siasa vimekaguliwa baada ya kuwasilisha taarifa zao za hesabu ambazo zitawasilishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa katika vikao hivyo vya Kamati ya Bunge hivi karibuni.

Aidha, alisema ripoti hiyo ilibainisha kuwa katika uuzwaji wa kampuni ya Southern Paper Mills (SPM) kwa kampuni ya Rai Group ya Kenya kuna baadhi ya taratibu hazikufuatwa lakini kampuni hiyo ya Kenya inamiliki SPM kwa asilimia 100.

Zitto, aliitaka ofisi hiyo ya CAG kuhusu hati hizo chafu kuhakikisha inazitoa kila mwaka hadi pale Serikali itakapofuata viwango hivyo vya kimataifa kwa kuandaa hesabu kulingana na matakwa hayo ya kimataifa na kuhusisha taasisi na mashirika yake yote ya umma.

Aidha, aliagiza kamati yake ipatiwe orodha ya bohari zote za forodha nchini zinazofanyakazi bila leseni ili ziweze kufanyiwa kazi na kubainika kiasi gani cha fedha kinachopotea.

“Lakini leo (jana) tumepokea upande huu wa CAG kesho (leo) tunakutana na upande wa Serikali ambao haya yote utayajibu,” alisema Zitto.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: