BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC YADORORA MBELE YA KLABU YA WITS UNIVERSITY YA AFRIKA KUSINI NA KUTANDIKWA BAO 4-2.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJYOCAbOjuloh2sT0AmqIjDBp2ZJVt2h_ynHui2vF6vIBcEMV-R_0JV1mfNMSqb5otWpZxMiiQmv2ZB_juaZ-HhD5PKqM4vVFOobzjpODhsj3Bq2awMn7E95QBJY9TfVTcga2Vsb38qlq6/s400/1.JPG

SIMBA SC imefungwa mabao 4-2 na Wits University katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Starock Park mjini Johannesburg, Afrika Kusini.


 

Kipa wa tatu, Peter Manyika kwa dakika zote ndiye aliyekuwa langoni akitunguliwa mara nne, wakati mabao ya Simba SC yakifungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ na Elias Maguri.


Pamoja na kufungwa 4-2, Simba SC imecheza soka ya kuvutia na kocha Patrick Phiri ameridhishwa na kiwango, akisema anakwenda kufanyia kazi makosa yaliyojitokeza leo.

Huo ni mchezo wa pili kwa Simba SC katika kambi yake ya Afrika Kusini ya takriban wiki mbili tangu wiki iliyopita kujindaa na mechi dhidi ya mahasimu Yanga SC Oktoba 18, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali, Simba SC ilitoka sare ya 0-0 na Orlando Pirates Jumamosi wakati kesho itamemyana na Jomo Cossmos na Jumatano itacheza na SuperSport, pia ya Afrika Kusini.


Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdul Aziz, Joseph Owino, Pierre Kwizera, Twaha Ibrahim ‘Messi’, Abdallah Seseme, Elias Maguri/Ibrahim Ajibu, Shaaban Kisiga ‘Malone’/Amisi Tambwe na Uhuru Suleiman/Ramadhani Singano ‘Messi’.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: