TANZANIA inakabiliwa na upungufu wa wataalam wa upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo kwa sasa ina madaktari watano ambao wanazunguka katika hospitali za rufaa nchini kutibu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk. Othman Kiloloma katika maadhimisho ya siku ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kimataifa
Dk. Kiloloma alisema kwa kuwa tatizo la watoto wanaozal;iwa na ugonjwa huo ni kubwa, wataalam wa kutibu tatizo hilo wanapaswa kuwa wengi ili waweze kujigawa katika hospitali za rufaa ambazo zinatoa huduma hiyo.
Alisema madaktari hao watano pamoja na wataamu wengine kutika nje ya nchi, hutibu watoto 200 kwa mwaka, idadi aliyodaikuwa ni ndogo sana kulingana na mahitaji.
“Ingawa hospitali za rufaa za MOI, KCMC na Bugando zinazotoa huduma hii kupokea watoto wengi wenye tatizo hilo, bado watoto wengi wapo vijiji …wanashindwa kuletwa kutokana na gharama kubwa za usafiri na kujikimu wawapo wodini” alisema Dk. Kiloloma
Naye Daktari bingwa wa magonjwa hao, Hamis Shaban alisema watoto wanaopata tatizo hilo, wengi wao uwa walelamavu wa miguu kutokana na kukosa nguvu, wengine upata utapiamulo na kushambuliwa na magonjwa tofauti kutokana na lishe wanayopata.
Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, Abdulhakim Bayakub, alisema takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya 100 upoteza maisha kila mwaka kutokana na wazazi wao kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina.TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment