MTANZANIA KUCHUANA KATIKA SOKA NA MSHAMBULIAJI WA JUVENTUS CALORS TEVEZ LIGI KUU YA ITALIA "SERIE A".
MSHAMBULIAJI Haji Ungando ametua katika timu ya Atalanta inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Italia ‘Serie A’, kufanya majaribio ya siku 10 baada ya timu hiyo kuvutiwa naye.
Kinda huyo akifanikiwa kusajiliwa na Atalanta inayoshika nafasi ya 17 Serie A, ataungana na washambuliaji wakubwa duniani kama Carlos Tevez (Juventus), Gonzalo Higuain (Napoli), Francesco Totti (Roma) wanaokipiga kwenye ligi hiyo.
Mmiliki wa kituo cha kukuza vipaji cha Jaki Sports Academy, Jamal Kisongo, aliliambia MTANZANIA jana tayari Ungando ameshafika Italia toka juzi alasiri, ambapo kuanzia jana alitarajia kutazamwa na timu hiyo inayonolewa na Muitaliano Edoardo Reja.
“Ameshafika huko na wamempokea vizuri na kuanzia leo (jana) wataanza kupata taarifa zake kwa kina kuhusu majaribio yake ya siku ndani ya timu hiyo na tunazidi kumuomba Mungu afanikiwe ili afungue milango kwa Watanzania wengine huko,” alisema.
Alisema straika huyo alikuwa akilelewa na kituo chake na msimu uliopita walimpeleka kwa mkopo nchini Kenya kwenye timu ya Nakuru, kabla ya kurejea tena nchini na hatimaye kupata dili hilo.
Ndani ya kikosi cha Atalanta kuna washambuliaji wengine wakali kama Rolando Bianchi aliyewahi kukipiga katika Ligi Kuu England wakati akiwa na miamba ya huko Manchester City, huku kikiwa na mchezaji mmoja tu kutoka Afrika ambaye ni Mghana, Richmond Boakye.
0 comments:
Post a Comment