Nchi za Afrika Mashariki na kati ikiwamo Tanzania zipo katika wasiwasi wa kukumbwa na mvua za El-nino kutokana na kuongezeka kwa joto katika Bahari ya Pacific.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk. Agness Kijazi.
Alisema mkutano huo unawahusisha wataalam mbalimbali kutoka katika nchi 11 na unaangalia mifumo ya hali ya hewa kwa Afrika Mashariki na tayari wameona viashiria vya kutokea kwa mvua hizo.
“Mvua hizo hutokea pale kiwango cha joto kinapoongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye bahari na mpaka sasa tumeona joto limeongezeka kwa kiasi kikubwa katika bahari ya Pacific,” alisema Kijazi.
Alisema baada ya kuangalia mifumo ya hali ya hewa katika eneo la Afrika Mashariki, wataalamu watarudi katika nchi zao na kuangalia mifumo ya hali ya hewa katika maeneo yao na kutoa utabiri kwa wananchi husika kwa kipindi Septemba mpaka Desemba.
Kijazi alitoa wito kwa wananchi na wadau wa hali ya hewa kufuatilia utabiri utakaotolewa Septemba Mosi, mwaka huu ili kujua hali itakavyokuwa. CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment