BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NYERERE AMNANGA MGOMBEA URAIS WA UKAWA EDWARD LOWASSA NA FREDIRICK SUMAYE KWA KUHAMIA UPINZANI.

 
Mhe Makongoro Nyerere.

Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, wakati wasanii mbalimbali wakitumbuiza katika uzinduzi huo, alikuwa aliwapiga vijembe vyama vinavyounda na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwamba vimebeba makapi akidai kuwa wanadhani watangia Ikulu.

Nape alikuwa akimaanisha makapi ni waliokuwa makada wa CCM ambao wamekihama chama hicho kwa nyakati tofauti na kujiunga upinzani vya Chadema, na NCCR- Mageuzi na CUF.

Miongoni mwa makada hao walitimkia Ukawa ni waliokuwa mawaziri wakuu, Edward Lowassa (Chadema) na Frederick Sumaye (NCCR-Mageuzi).

Baada ya Lowassa kujiunga na Chadema, aliteuliwa kuwania urais akiwalisha Ukawa wakati Sumaye juzi baada ya kuhama CCM alisema amekwenda kuimarisha upinzani.

MAKONGORO NYERERE
Naye Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Makongoro Nyerere, aliponda makada wa CCM waliohamia upinzani wakiwamo Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

Akizungumza katika mkutano huo, Makongoro ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara tangu mwaka 2007 hadi 2012, alidai kuwa Sumaye siyo mkweli kwani alipokuwa CCM alinukuliwa akisema iwapo chama hicho kitamteua Lowassa kugombea urais kwa angekihama.

“Wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea urais Sumaye alisema hiki chama mkimpa Lowassa, atahama chama kwa kuwa tunamweshimu Sumaye hatukumpitisha Lowassa, lakini bado amehama na kwenda kumkumbatia fisadi,” alisema.

Alisema pale ambako mtu hazumgumzi ukweli anaitwa mwongo, hivyo kauli yake hiyo Sumaye hana tofauti na mwongo kwani katika kipindi cha miaka kumi iliyopita aliingia katika kinyang’anyiro cha urais na alifika tano bora, lakini kura hazikutosha badala yake zikatosha za Kikwete.

Alisema miaka kumi baadaye Sumaye ameingia katika kinyang’anyilo cha urais bahati mbaya hakuingia katika tano bora, lakini cha kushangaza anaanza kuishukutumu CCM kwamba ni chama kibaya wakati alipoingia tano bora alikisifia.

“Mnaufahamu mchezo wa chandimu, ambao huchezwa na vijana tu na mzee akiingia akija anataka nini?alihoji na kuongeza;

“Sumaye kaingia katika mchezo huu wa chandimu mwenyewe, tutamsema.”

Mbali na Sumaye na Lowassa, wapinzani wengine waliohama CCM na kuiunga na upinzani ni wagunge waliomaliza muda wao wa Kahama, James Lembeli; Viti Maalum, Ester Bulaya; Arumeru Magharibi, Ole Medeye; Segerea, Dk. Makongoro Mahanga na wa Sikonge, Said Mkumba.

Wengine ni wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Arusha, Onesmo Ole Nangole; Singida, Mgana Msindai na Shinyanga, Khamis Mgeja pamoja Mwenyekiti wa zamani wa Dar es Salaam, John Guninita.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: