VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA VYASHIRIKI KIKAMILIFU USAFI MOROGORO
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akifyeka nyasi na askari wa jeshi la polisi ndani na nje ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa kufagia, kufyeka nyasi na kuzoa takangumu ikiwa ni sehemu ya maazimisho ya sherehe za miaka 54 ya Uhuru iliyoadhimishwa nchini kote kwa watumishi mbalimbali kufanya usafi wa mazingira. Picha na MTANDA BLOG.
Askari wa Chuo cha Mafunzo ya Huduma Pangawe JWTZ wakifanya usafi wa kufyeka nyasi eneo linalozunguka hospitali ya mkoa wa Morogoro katika maadhinisho hayo.Picha na MTANDA BLOG.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo akifagia takangumu pamoja na askari wa jeshi la polisi ndani na nje ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro. Picha na MTANDA BLOG.
Juma Mtanda,Mwananchi
Morogoro.Vikosi vya ulinzi na usalama vilivyopo mkoani Morogoro vimeshiriki kikamilifu katika sula la usafi ambapo vilifanya usafi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na Ikulu ndogo.
Akizungumza na gazeti hili mjini hapa, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paoulo alieleza kuwa zoezi hilo walianza majira ya saa 12 asubuhi kwa kufanya usafi ndani na nje ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
“Sisi kama jeshi imekuwa ni desturi yetu kufanya usafi na tumekuwa tukifanya usafi katika makazi yetu lakini tumeitikia wito wa rais wa kufanya Desemba 9 kama maadhimisho ya uhuru,”alisema Paulo.
Vikosi vilingine vilivyofanya usafi katika hospitali hiyo ni askari wa kikosi cha JWTZ kambi ya Pangawe kilichokuwa kikiongozwa na makapteni, Joseph Narsis na David Minga huku askari wa jeshi la Magereza wakifanya usafi ikulu ndogo.
Maeneo mengine ya umma yaliyofanyiwa usafi wa mazingira ni pamoja na hospitali ya wilaya ya Sababa, soko kuu la mkoa wa Morogoro,soko la mawenzi.
Diwani wa kata ya Sabasaba, Mudhihiri Shoo aliongoza timu ya watu katika kata yake kufanya usafi katika hospitali ya Sabasaba kwa kujumuisha vijana wa skauti, wakazi wa kata hiyo, wafanyakazi wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Morogoro, watumishi wa hospitali na wanafunzi wa chuo kikuu huria tawi la Morogoro.
0 comments:
Post a Comment