BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HOTELI YA STAR COM KITONGA YAFUNGWA KWA KUKITHIRI KWA UCHAFU IRINGA



Iringa. Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imeifunga hoteli inayotumiwa na wasafiri wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Mikoa hiyo ni Iringa, Mbeya, Songea, Songwe na Katavi

Hoteli hiyo ya Star Com iliyopo katika Mlima Kitonga wilayani humo kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo kutiririsha maji machafu kwenye mto Lukosi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Star Com, Henry Vegele amesema kuwa walipokea barua ya notisi ya siku tano kutoka katika halmashauri hiyo ikiwataka kufanya marekebisho katika maeneo mbalimbali na tayari wameyafanya.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dk John Mwingira ameliambia gazeti hili kuwa hoteli hiyo imekuwa ikitiririsha maji hayo kutokana na chemba za kuyahifadhia kuwa ndani ya mita 60 kutoka kwenye mto huo.

“Ni kweli tumeifunga ile hoteli kwa muda hadi hapo watakapokamilisha kufanyia marekebisho maelekezo ya idara ya afya, tumeshauri ahamishe ili asiendelee kuchafua maji yale ambayo yanatumiwa pia na wananchi,” amesema Mwangira.

Mambo mengine yaliyosababisha hoteli hiyo ifungwe ni kutopakwa rangi katika eneo la jiko, kutokuwa na marumaru eneo hilo pamoja na kurekebisha miundombinu ya mitaro ya maji.

Wakati uongozi wa halmashauri ukitoa taarifa hiyo baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa hoteli hiyo kwa kuuza bidhaa ndogo ndogo zikiwamo nyanya, vitunguu na mbogamboga wameiomba kuifungua kwa kuwa familia zao zinataabika na njaa.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: