BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HAKUNA RUHUSA KWA WAISLAMU KUUPOKEA MWEZI WA RAMADHANI KWA KUVUNJA JUNGU



Dar es Salaam. Waislamu nchini wametakiwa kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya matendo yaliyo mema yanayoendana na amri za Mwenyezi Mungu.


Kauli hiyo imetolewa na Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum wakati wa kufungua mafunzo ya viongozi wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (Juwakita-Bakwata) kutoka mikoa ya Kanda ya Mashariki.


“Kuna namna ya kuupokea mwezi huu Mtukufu, kwanza tuupokee kwa matendo yaliyo mema, kuna neno limezoeleka katika jamii kuwa eti kuvunja jungu. Maana yake ni kutenda dhambi za mwisho mwisho…nasema kitendo hicho ni kinyume na dini ya Kiislam,” amesema Shekhe Salim na kuongeza:


“Ninawaomba watu waache tabia ya kualika na kualikana katika kumbi mbalimbali za starehe kwa lengo la kwenda kuvunja jungu, hili jambo sio jambo zuri kwani mwezi Mtukufu wa Ramadhani haukaribishwi kwa matendo maovu bali unakaribishwa kwa matendo mema yanayompendeza Allah.”


Katika ufunguzi huo, kiongozi huyo wa dini amewahimiza Watanzania nchini kupendana, kusaidia na kuacha matendo maovu ambayo yanakwenda kinyume na amri za Mungu.


Awali Mwenyekiti wa Juwakita-Bakwata, Shamim Khan alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi jumuiya hiyo ili nao waende kuwaelimisha viongozi wa wilaya katika mikoa hiyo.


Naye Katibu Mkuu wa Juwakita, Hajati Mwatumu Malale amewataka wanawake wa Kiislam na wale ambao sio wa Kiislam nchini kuwa na nidhamu katika mambo wanayofanya ikiwemo kupendana na kusoma kwa bidii.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: