Mbeya. Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, jana ilivitaja vipodozi hatarishi kutumiwa na wajawazito.
Ilisema vipodozi hivyo vilishapigwa marufuku kuingizwa nchini, lakini vinauzwa kinyemela na wafanyabiashara wasio waaminifu.
Kaimu Meneja wa TFDA Nyanda za Juu Kusini, Rodney Alananga, alivitaja vipodozi hivyo kuwa ni
Carolite, Betason, Boss Lotion, Extra Clair, Skin balance Lemon, Top lemon, Lovely body na sabuni ya Jaribu.
Alisema vikitumiwa na wajawazito licha ya kuwaathiri wao, pia huweza kusababisha mtoto aliyeko tumboni akapatwa na mtindio wa ubongo.
0 comments:
Post a Comment