Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonventura Mushongi alieleza kuwa watu wawili walikamatwa na gari hilo wilayani humo katika barabara kuu ya Bagamoyo-Dar es Salaam.
Mushongi aliwataja waliokamatwa na gari hilo kuwa ni Ezekiel Daudi (25), mfanyabiashara na mkazi wa Moshi aliyekuwa kwenye gari hilo huku aliyekuwa anaendesha Joshua Eliya Adam akitoroka lakini Daudi analisaida Jeshi la Polisi kuhusu tukio hilo.
"Tulitega mtego ambao uliowekwa na Jeshi letu la Polisi kwenye barabara kuu ya Bagamoyo-Msata, Kata ya Kiwangwa usiku wa juzi na uliwezesha kunaswa kwa wezi pamoja na gari hilo waliloiba".alisema Kamanda Mushongi.
Kamanda Mushongi alisema kuwa watu hao waliiba gari hilo aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T400DEH ikiwa ni mali ya ofisa afya wa JWTZ ambaye alikuwa akifanya kazi katika Hospitali ya Lugalo na kwa sasa amehamishiwa Darfur nchini Sudan ingawa sasa yuko mapumzikoni jijini Dar es Salaam.
Lile gari wakati gari linaibwa ndani yake kulikuwa na watoto wawili, lakini walimshusha mmoja wa kiume, Phillip na kuondoka na mwingine wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, Lightness Dallu.aliongeza Kamanda Mushongi.
0 comments:
Post a Comment