Mchezaji wa Mtibwa Sugar, Ally Makalani (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe (katikati) na mlinzi Mwinyi Haji wakati wa mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. (Picha na Mroki Mroki
MAMBO yalikuwa shwari kwa Simba na Yanga jana, baada ya kushinda mechi zao za Ligi Kuu zilizochezwa kwenye viwanja viwili tofauti.
Vinara wa ligi hiyo, Simba wakiwa ugenini Mbeya walichomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mjini humo.
Ushindi wa Simba umeifanya kujikita kileleni ikiwa na pointi 20 katika mechi zake nane ilizocheza. Mashujaa wa Simba jana walikuwa Ibrahim Ajib aliyefunga bao la kuongoza katika dakika ya 6, baada ya kupiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja golini.
Dakika ya 33, Shizza Kichuya aliifungia Simba bao la pili baada ya kuwachambua mabeki wa Mbeya ambao walionekana kupwaya tangu mwanzo wa mchezo.
Simba ingeweza kupata bao la tatu lakini mchezaji wake, Fredrick Blagnon alikosa mkwaju wa penalti iliyopanguliwa na kipa wa Mbeya City ambapo mchezo huo Simba haikumchezesha mshambuliaji wake Mavugo aliyesuasua katika michezo kadhaa ya ligi kuu bila kuvumania nyavu na kukaa benchi katika mchezo huo.
Kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, mabingwa watetezi Yanga walichomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 14 kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi saba. Mabao ya Yanga jana yalifungwa na Obrey Chirwa katika dakika ya 45 akiunganisha mpira wa Simon Msuva na kuujaza mpira wavuni.
Mtibwa Sugar ilisawazisha bao hilo katika dakika ya 63 kupitia kwa Haruna Chanongo, lakini lilidumu kwa dakika tano tu kabla Msuva hajaiongezea Yanga bao la pili katika dakika ya 68 na Donald Ngoma kuongeza bao la tatu katika dakika ya 79.
Kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga, Stand United iliendelea kushangaza mashabiki wa soka baada ya kuifunga Azam bao 1-0.
Ushindi huo unaifanya Stand kuendelea kukaa kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 katika mechi tisa ilizocheza.
Kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, Toto Africans ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa timu ngeni kwenye ligi Mbao FC.
Mbao ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza katika mechi hiyo kwenye dakika ya 39 kupitia kwa Dickson Ambundo kabla Waziri Junior hajaisawazishia Toto katika dakika ya 41.
Mbao ilianza kipindi cha pili kwa kasi na katika dakika ya 58 Hussein Swedi aliiandikia bao la pili kabla Boniface Maganga hajaongeza bao la tatu katika dakika ya 90.
Mechi nyingine ilichezwa jana kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi ambapo wenyeji JKT Ruvu walitoka suluhu na Prisons.Habarileo
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / michezo /
slider
/ MAVUGO SI LOLOTE NDANI YA KLABU YA SIMBA SC AKALIA BENCHI DHIDI YA MBEYA CITY.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment