BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIRI YA ONGEZEKO LA KUACHIKA KWA WANAWAKE KATIKA NDOA KWA KUPEWA TALAKA KWAFICHUKA

 
Mabadiliko ya tabia, mila, silka na utamaduni kwa vijana yametajwa kuwa chanzo kikuu cha ongezeko la talaka visiwani hapa.

Wakizungumza katika mkutano wa mapitio ya Sheria ya Mahakama ya Kadhi na Sera ya Jinsia, washiriki walisema ni lazima ifike pahali itafutwe njia ya kurejesha maadili hayo.

Akizungumza katika mkutano huo, Mussa Abdallah Mussa alisema maadili kwa vijana yamepungua na kusababisha talaka nyingi.
Alisema kutokana na hali hiyo, ipo haja ya kuangalia kwa kina mahali walipojikwaa ili kuondoa tatizo hilo.

Mkurugenzi wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zafela), Jamila Mahmoud, alisema katika Sheria ya Mahakama ya Kadhi, kuna mapungufu kadhaa ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho.

Alisema chini ya sheria ya sasa, hakuna kifungu maalumu cha mgawanyo wa mali kwa wanandoa wanapoachana ambalo ni tatizo kubwa kwa wanawake wa Zanzibar.

Alisema hilo linachangia kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia unaowakabili zaidi wanawake.
Aidha, alisema katika sheria ya sasa hakuna ufafanuzi wa mali kwa wanandoa kitu ambacho ni hatari kwa mwanamke pale anapopewa talaka.

Mapungufu mengine aliyoyataja ambayo yamo katika sheria hiyo ni utaratibu wa Mahakama Kuu kuongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu na Maulamaa wanne pale inaposikiliza rufani kutoka Mahakama ya Kadhi.

Alisema ingawa masharti hayazuii wanawake kuteuliwa kama Ulamaa, lakini kwa Zanzibar hakuna mwanamke hata mmoja aliyewahi kuteuliwa kuwa Ulamaa.

Kwa mujibu wa Jamila, hii ni tofauti na nchi nyingine kama Malaysia na Indonesia ambako wanawake wanateuliwa kuwa Ulamaa.Nipashe


Jamila aliongeza kuwa sheria ya sasa inahitaji wanandoa na shahidi wao kwenda kwa msajili ili kusajili ndoa ndani ya siku 14, lakini haizungumzii talaka na kuomba sheria hiyo mpya izungumzie usajili wa talaka pia ili iwe rahisi utafutwaji wa haki na upatikanaji wake.


Alisema pungufu lingine waliloliona ni kutoruhusiwa kwa wakili katika Mahakama ya Kadhi, hali ambayo inahatarisha haki kupatikana kwa wanawake wengi na ni kinyume cha haki.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: