BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAWAKE WAMTIBULIA DONALD TRUMP MBIO ZA URAIS MAREKANI, HAPANDWI NA MKEWE


Viongozi wakuu wa chama cha Republican wanazidi kuondoa uungaji wao mkono kwa Donald Trump (pichani juu) kwa matamshi yake ya kuwadhalilisha wanawake. John McCain

Miongoni mwa wanasiasa wa hivi punde zaidi ni pamoja na aliyekuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice, na aliyegombea kiti cha urais nchini humo, Senator John McCain.

Lakini Trump amesema kwamba hatajiondoa kutoka katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti hicho licha ya malalamishi kutoka kote duniani kutokana na matamshi yake ya kuudhi kuwahusu wanawake, aliyo-yatoa mwaka 2005.

Zaidi ya wanasiasa 24 wa chama chake cha Republican, sasa wamesema hadharani kuwa hawamuungi mkono bilionea huyo na wanamtaka kumuachia mgombea mwenza, Mike Pence nafasi ya kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa Marekani hapo mwezi Ujao.

Miongoni mwa wanaolaani matamshi hayo ya Trump ni pamoja na mkewe Trump- Melania. Aliyekuwa waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Condoleezza Rice

Amesema kuwa licha ya kuendelea kumuunga, analaani matamshi hayo mapotovu dhidi ya wanawake.

Spika wa Bunge Paul Ryan, alizomewa na kushangiliwa kwa wakati mmoja, katika mkutano mmoja wa kisaiasa baada ya kukataa kutumia jukwaa moja na Trump.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: