BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAWAKE WALIVYOHAMASISHWA KUPANDA MITI KATIKA VYANZO VYA MAJI WAKATI WA WIKI YA MAJI MOROGORO


Kaimu Afisa wa Maji Bodi la maji bonde la Wami-Ruvu, Grace Chitanda akizindua kwa kupanda mti huku Mbunge wa viti maalumu Chadema mkoa wa Morogoro, Devotha Minja (aliyesimama nyuma yake) wakati wa zoezi la upandaji miti ili kurejesha uoto wa asili kando mwa bwawa la mindu katika kampeni ya kuhamasisha wanawake kutunza mazingira katika vyanzo vya maji Morogoro
mwishoni mwa wiki ambapo jumla ya miti zaidi ya 4000 ilipandwa.. PICHA ZOTE/MTANDA BLOG

Mbunge wa viti maalumu Chadema mkoa wa Morogoro, Devotha Minja akishirikiana kupanda mti na Jesca Patrick aliyembeba mtoto wake, Grace Dickson (1) wakati wa zoezi hilo la upandaji wa miti ili kurejesha uoto wa asili kando mwa bwawa la mindu.

Mbunge wa viti maalumu Chadema mkoa wa Morogoro, Devotha Minja na mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communications Morogoro, Hamida Shariff wakishirikiana kupanda mti wakati wa zoezi hilo.

Halfan Diyu, mwandishi mkongwe gazeti la Majira akipanda mti katika tukio ikiwa kuwaunga mkono juhudi wanawake katika
upandaji miti na kurejesha uoto wa asili kando ya bwawa la mindu.

Hapa Mhe Devotha Minja akipanda mti kwenye zoezi hilo la upandaji miti.

Ashura Kazinja kushoto na Christina Haule (katikati) wakimhoji mmoja wa wanawake walioshiriki zoezi la upandaji wa miti.

Mfanyabiashara, Tito Haule naye hakuwa nyuma katika juhudi ya kuwaunga mkono wanawake, hapa akionekana akiwa ameshika miche ya miti tayari kwa kupanda.

Mmoja wa mwanamke akishiriki kupata mti.



Mhe Minja akizungunza jambo kabla ya zoezi la upandaji miti kuanza.

Hapa Mhe Devotha Minja akiwa na baadhi ya wanawake wakielekea kwenye eneo husika la kupanda miti
Baada ya kazi kumalizika: Sehemu ya wanawake wa Manispaa ya Morogoro wakiongozwa na Hamida Shariff wa kwanza kushoto akichuma mlenda mgunda katika shamba mara baada ya zoezi la upandaji miti kumalizika mwishoni mwa wiki ambapo jumla ya miti zaidi ya 4000 ilipandwa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: