NI MANENO YA HEKIMA LAKINI KUNA HEKIMA YA KUJIFUNZA HAPA !.
Na Bashir Nkoromo.
Palikuwa na mchoraji mmoja kwenye moja ya mji na mchoraji huyo alikuwa mwenye umri wa utu uzima na ujuzi wa hali ya juu katika fani hiyo.
Picha alizokuwa akichora zilikuwa nzuri sana na akiuza kwa gharama kubwa sana na kumpatia fedha za kutosha.
Siku moja maskini na mafukara walikwenda kwenye mji ule hadi eneo alilokuwa anachora na kumwambia hivi.
"Ewe ndugu, unatengeneza kipato kikubwa sana kwa kazi yako hii, lakini kwa nini hutaki kutusaidia sisi watu wa hali ya chini ?.walisema mmoja wao.
wakaendelea kusema kuwa watazame wenzako wanaouza nyama, ijapokuwa hawana kipato kikubwa lakini kila siku hutoa vipande vya nyama kuwasaidia wasiojiweza wakimaanisha wao.
Huyu mchoraji hakuwajibu neno lolote, isipokuwa alinyanyua macho na kuwaangalia wale maskini kwa huzuni, kisha akainama kichwa chini.
Wale mafukara wa mji ule waliondoka wakichukizwa na suala lile la mchoraji kukaa kimya pasina kuwajibu.
Wale mafukara na masikini ikawa wakitangaziana pale kijijini kuwa yule mchoraji mwenyezi mungu amemjaalia kipato kizuri lakini ni mbahiri si mwenye kuwasaidia wasiojiweza.
Baada ya muda, yule mchoraji alianza kuugua na hakuna mwanakijiji yeyote aliyekwenda nyumbani kwake kumuona mpaka akafa.
Baada ya kufa yule mchoraji siku zilipita, lakini cha ajabu wale wauza nyama wakawa hawagawi tena nyama kwa masikini jambo lililowastua na kulazimika kwenda kuwauliza kulikoni ?.
Wakaenda kuwauliza wale wauza nyama ni kwanini hawasaidii tena nyama kama walivyokuwa wanafanya zamani.?
Wauza nyama wakawajibu kuwa yule mchoraji ndiye aliyekuwa akiwapa pesa wao wauza nyama kila mwezi kwa niaba ya kuwanunulia nyama wasiojiweza.
Na wawape bure kila siku lkn alipofariki likasimama jambo hilo kwani hazikutoka tena pesa za kuwanunulia wao nyama kwa kuwa mchoraji ameshakufa.
SOMO NDILO HILI.
Baadhi ya watu huenda wakawa wanakudhania vibaya lakini na wengine huenda wakakuona msafi kama maji yasiyoharibiwa.
Tambua hawakuzidishii kitu kwa wao kukuona wewe kuwa ni msafi
na wala hawakupunguzii kitu kwa wao kwa kukudhania vibaya.
Kilichomuhimu ni vile akujuavyo mola wako kuwa ww ni mtu wa aina gani kwani yy ndiye anaejua ya siri na ya dhahiri.
Usimuhukumu mtu yeyote kwa muonekano wake wa nje kwani hujui undani wake.
Kwani hujui undani wake kuna baadhi ya matendo ayafanyayo lau kama ungeliyajua ungemuhishimu sana.
0 comments:
Post a Comment