Munge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali akizungumza jambo na askari polisi.
Juma Mtanda, Morogoro.
Mbunge wa jimbo la Kilombero Chadema, Peter Lijualikali amekamatwa na maafisa wa polisi ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kuhairishwa kwa kesi yake yenye mashtaka nane likiwemo la kuchoma moto ofisi ya kijiji.
Lijualikali alikamatwa ndani ya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro na maafisa hao na kupelekwa kwenye kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro kwa kile kilichodaiwa na maafisa hao kuwa wanataka kumhoji mbunge huyo.
Munge huyu baada ya kuingiza kwenye gari la polisi aina ya Landcruser lenye namba maalumu BOT 164 V, gari hilo liligoma kuwaka na hivyo maafisa hao walilazimika kulisukuma na baadaye maafisa hao walilazimika kumhamisha na kumuingiza kwenye gari jingine la polisi hilo.
0 comments:
Post a Comment