wa Tanzania Prinson, David Mwanjika kulia wakati wa fainali ya ligi
daraja la kwanza hatua ya tisa bora katika uwanja wa Jamhuri Morogoro
katika mchezo huo Prinson ilikubali kipigo cha bao 2-0.
Mshambuliaji wa klabu ya Rhino FC, Amri Sambiga kulia akichuana na mlinzi wa Polisi Dar, Vicent Dumiwe kushoto wakati wa mechi za ufunguzi ligi daraja la kwanza hatuia ya tisa bora katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro katika mchezo huop ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Baadhi ya waandishi wa habari wakijadiliana jambo wakati wa ligi daraja hatua ya tisa bora uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mshambuliaji wa kalbu ya Mlale JKT, Igogo Maganga kushoto akiwania mpira dhidi ya George Akitanda wa JKT Mgambo Shooting wakati wa ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora uwanja wa Jamhuri Morogoro katika mchezo huo Mgambo walishinda bao 3-0.
KLABU ya Polisi Morogoro Sports Club wameanza vema ligi daraja la kwanza hatua ya 9 bora baada ya kuitandika Tanzania Prinos ya Mbeya kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Mabao ya Polisi Moro SC yalifungwa katika kipindi cha kwanza kupitia kwa wachezaji wake Juma Lazio dakika ya 11 akiunganisha krosi ya mshambuliaji Iman Mapunda kabla ya Ally Shariff kufunga bao la pili dakika ya 31 baada ya golikipa wa Prinson, Ibrahim Shabaan kutema shuti kali la mshambuliaji Nicolaus Kabipe na mpira huo kumkuta mfungaji aliyefunga bao hilo la ushindi kwa Polisi Moro SC.
Prinson waliingia kipindi cha pili kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi katika lango la Polisi Moro SC likini washambuliaji wake walikosa umakini wa kufunga hasa kutokana na vikwanzo ikiwemo mlindamlango Kondo Salaam na walizni wa timu hiyo.
Katika michezo mingine iliyofanyika kwenye ufunguzi Mbeya City FC waliitandika timu ya Transit Camp kwa bao 3-0.
Ligi hiyo ambayo inashirikisha klabu tisa za Mgambo Shooting FC, Tanzania Prinson, Polisi Dar es Salaam, Transit Camp, Rhino Rangers FC, Polisi Tabora, Mbeya City FC, Mlale JKT na wenyeji wa mashindano hayo Polisi Moro SC yanatarajia kutoa timu tatu za juu ambazo zitaingia kucheza ligi kuu ya vodacom Tanzania bara msimu ujao.
Katika mchezo huo vijana hao wanaonolewa na kocha, Juma Mwambusi walionyesha nia ya kupata pointi tatu muhimu hasa katika mchezo huo wa ufungizi baada ya mshambuliaji wao Ipiana Samson kuiandikia bao la mapema dakika ya tisa kufuatia mlinda mlango wa Transit Camp, Abdulkarim Mtumwa kuokoa mchomo wa mshambuliaji wa Mbeya City FC kabla ya kukwamisha mpira huo kimiani kwa kichwa akiwa eneo la sita na kuandika bao la kuongoza.
Baada ya kupata bao hilo Mbeya City FC walicharuka na kuendeleza mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la wapinzani wao huku wakiwa wameteka eneo la kiungo hali ambayo ilimpa mwanya mshambuliaji, Mwagane Yeya kufunga mabao mawili ikimo la pili na tatu aliyofungwa katika dakika ya 59 na 85.
Mshambuliaji huyo, Mwagane Yeya alifunga mabao hayo baada ya ushirikiano mzuri na kiungo mshambuliaji Patrick Mangunguli kwa bao la pili huku bao la tatu akishirikiana vema na mchezaji Francis Casto na kufanya mchezo huo umalizike kwa Transit Camp kupoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 3-0.
Katika mchezo uliochezwa majira saa 8 mchana Polisi Dar es Salaam ililazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Rhino Rangers katika mchezo mkali na kusisimua uliofanyika kwenye uwanja huo huo wa jamhuri.
Rhino Rangers ndiyo walianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Shija Mbongo dakika ya 26 baada ya krosi ya winga ya kushoto Venance Genda na kumkuta mfungaji aliyepiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni likimwaacha mlinda mlango wa Polisi Dar es Salaam Akbiri Babu asijue la kufanya na kuandika bao kwa Rhino Rangers.
Polisi Dar es Salaam walisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji Patrick Mrope dakika ya 72 akifungwa kwa njia ya kichwa baada ya kuunganisha krosi ya Paul Barnabas na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Nayo klabu ya JKT Mgambo Shooting iliitandika Mlale JKT kwa bao 3-0 kwa mabao ya washambuliaji Fully Maganga aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 52 na 88 baada ya kushirikiana vizuri na wachezaji wenzake Chande Magoja kwa bao la pili wakati bao la kwanza akifunga baada ya uzembe wa mlinda mlango wa Mlale JKT Vita Manyika na bao lingine lilifungwa na Chande Magoja dakika ya 84 huku Edward Malimi wa JKT Mlale akikosa penalti baada ya mchezaji wao kuangushwa kwenye eneo la hatari dakika 52.
0 comments:
Post a Comment