BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

LIGI DARAJA LA KWANZA HATUA YA 9 BORA JKT MGAMBO SHOOTING NA POLISI TABORA ZASHINDA.

KLABU ya JKT Mgambo Shooting iliitumia vizuri mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mlale JKT FC katika ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora baada ya kuibuka na ushindi wa bao 30 katika mchezo mkali uliofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Katika mchezo huo JKT Mgambo Shooting ilizidiwa kila idara huku wakati mwingi wakizuia mashambulizi kutoka kwa Mlale JKT FC huku nao wakitengeneza mashambulizi machache ambayo washambuliaji wao Fully Maganga na Chande Magoja walitumia vema nafasi walizopata kupachika mabao hayo 3-0.

Washmabuliaji Fully Maganga na Chande Magoja wa JKT Mgambo Shooting waliiwezesha timu yao kutoka kidedea huku Maganga akifumania nyavu mara mbili katika dakika ya 52 na 88 huku bao la tatu likipachikwa na Magoja wakati mshambuliaji wa Mlale JKT FC Edward Malimi akikosa penalty baada ya mchezji wa Mgambo kufanya madhambi katika eneo la hatari ambayo aliipaisha na kuikosesha bao timu yake.

NAYO klabu ya Polisi Tabora iliitambia Rhino Rangers kwa bao 1-0 katika mfulululizo ya ligi hiyo ya kutafuta mafasi kwa timu tatu za juu kutinga ligi kuu ya Vodacom msimu ujao 2012/2013.

Bao lpekee la Polisi Tabora lilifungwa na Kenneth Abeid dakika 76, kwa shuti kali akiwa nje ya 18 lililokwenda moja kwa moja wavuni na kumshinda kipa wa Rhino, Abdulkarim Mtumwa.

Rhino walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kutegeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini washambuliaji wake walikosa umakini kumalizia.
LEO kutakuwa mchezo baina ya Mbeya City FC dhidi ya ndugu zao Tanzania Prinson utaochezwa majira ya saa 8 mchana wakati jiono saa 10 kutakuwa na mchezo mungine baina ya Polisi Moro SC dhidi ya JKT Mgambo Shooting. 

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: