JESHI la
wanamaji la Kenya limevurumisha mizinga kadhaa katika mji wa bandari wa Kismayu
nchini Somalia.
Msemaji wa jeshi hilo, Cyrus Oguna alisema
mashambulizi hayo pia yamelenga uwanja wa ndege wa Kismayu.
Oguna alisema hatua hiyo ni mwanzo wa kuanza
mashambulizi kamili ya kikosi cha AU kwa lengo la kuukomboa mji huo kutoka
mikononi mwa wanamgambo wa Al-shabab.
Habari zinasema kuwa wanamgambo hao
wamejiweka tayari na kuongeza idadi ya wapiganaji wake ili kukabiliana na
vikosi vya AMISOM.
Kwa sasa Kismayu ndio mji wa pekee muhimu
unaodhibitiwa na wanamgambo hao.
Bandari ya Kismayu ni moja ya vitega-uchumi
muhimu kwa wanamgambo hao na iwapo utatwaliwa na AMISOM itakuwa pigo kubwa kwa
Al-shabab wanaotaka kuipindua serikali ya Somalia.
0 comments:
Post a Comment