MAHAKAMA nchini Misri imewahukumu kifo magaidi 14 na wengine wanne
kifungo cha maisha jela kwa kosa la kushambulia jeshi na maafisa wa
polisi katika rasi ya Sinai.
Watu hao ni wafuasi wa kundi moja la wanamgambo ambao wamepatikana na
hatia ya kuwaua maafisa watatu wa polisi, mwanajeshi mmoja na raia
katika mashambulizi yaliyofanywa mwezi Juni na Julai mwaka 2011.
Eneo la Sinai la Misri kwa muda mrefu limekuwa likikabiliwa na
matatizo ya kiuslama.
Mwezi Agosti mwaka huu jeshi la Misri lilianzisha
operesheni kali ya kuimarisha usalama kwenye eneo hilo baada ya watu
wasiojulikana kuuwa askari 16 wa mpakani wa Misri.


0 comments:
Post a Comment