
WAKUU wa Sudan wanasema watu kadha wamekufa kwenye shambulio lilofanywa
na wapiganaji dhidi ya wanajeshi wa serikali katika eneo la Darfur,
magharibi mwa nchi.
Afisa mmoja wa serikali alisema wanamgambo wanaounga mkono serikali
wameuliwa katika shambulio hilo la ghafla, karibu na al-Fasher, mji mkuu
wa jimbo la North Darfur.
Umoja wa wapiganaji - Sudanese Revolutionary
Front - ulisema ulifanya shambulio hilo na kuuwa wanajeshi wa serikali
na kuteka magari ya jeshi na silaha.
Baadhi ya makundi ya wapiganaji ya Darfur mwaka
jana yalitia saini mkataba wa amani na serikali ya Sudan, lakini makundi
mengine yanaendelea kupigana.

0 comments:
Post a Comment