RAIS Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa,
nchi yake na Iran zina historia kongwe ya mahusiano.
Kikwete
amesema hayo katika hafla fupi ya kupokea hati ya utambulisho ya balozi
mpya wa Iran nchini Tanzania na kueleza kuridhishwa kwake na mwenendo wa
kukua uhusiano baina ya Tehran na Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania
amesema kuwa, Iran ina nafasi muhimu mno kieneo na kimataifa na kwamba,
imepiga hatua kubwa katika nyuga mbalimbali hususan za kielimu na
kiteknolojia na kuongeza kuwa, ana matumaini nchi yake itaweza kustafidi
na uzoefu wa Iran katika nyanja mbalimbali.
Rais Kikwete amesema,
Tanzania iko tayari kustawisha zaidi uhusiano na Iran.
Kwa upande wake
Mahdi Agha Jaafari, balozi mpya wa Iran nchini Tanzania amesema Iran
imeazimia kwa dhati kabisa kukuza ushirikiano wake na Tanzania katika
sekta mbalimbali.

0 comments:
Post a Comment