BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS AHMADINEJAD: UMOJA NDIYO NJIA YA KUWAOKOA WAISLAM

 Ahmadinejad: Umoja, njia ya kuwaokoa Waislamu
RAIS Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, umoja na mshikamano wa Waislamu ndio njia pekee itakayoweza kuwaokoa na misukosuko mbalimbali. 

Akizungumza na kundi la wanasiasa, viongozi wa kidini na wasomi wa Pakistan mjini Islamabad, Rais Ahmadinejad ameongeza kuwa kuna ulazima wa kubainishwa kwa uwazi masuala ya kimsingi ulimwenguni. 

Ameongeza kuwa, watu wa Ulaya na Marekani na jamii yote ya mwanadamu inaishi chini ya ukandamizaji, dhulma na unyanyasaji. 

Akielezea njama zinazofanywa na maadui zenye shabaha ya kuleta hitilafu kati ya watu wote ulimwenguni, Rais wa Iran amesema kuwa, Wazayuni na Marekani wanafanya njama za kuibua mifarakano kati ya watu wote ulimwenguni ili waweze kufanikisha malengo na maslahi yao haramu.

 Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Rais Ahmadinejad amesema kuwa, Wazayuni na waitifaki wao na hali kadhalika Marekani wamekuwa dhaifu mno na kwamba wananchi wa Gaza wameweza kusimama kidete na hatimaye  kujipatia ushindi kwenye vita vya siku nane kati yao na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: