BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RONALD ASAIDIA UJENZI WA SHULE ZA GAZA.

 Las celebraciones de Cristiano Ronaldo
MSHAMBULIAJI machachari wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Christiano Ronaldo ametoa kitita cha euro milioni moja na nusu kwa ajili ya  ukarabati wa shule zilizoharibiwa vibaya na mashambulizi ya mabomu ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza. 

Hii si mara ya kwanza kwa Christiano Ronaldo kutoa misaada kwa wananchi wa Gaza, kwani mwaka jana pia alinadisha viatu vyake vya michezo na fedha zilizopatikana alizikabidhi kwenye taasisi ya Real Madrid kwa shabaha ya kusaidia shule za Gaza.  

Hadi sasa Taasisi ya  Real Madrid imeweza kujenga shule 167 katika nchi 66 duniani. 
Las celebraciones de Cristiano Ronaldo
Ronaldo alikuwa mchezaji ghali mno duniani katika historia ya mchezo wa kabumbu  baada ya kuhama klabu yake ya zamani ya Manchester United ya Uingereza na kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa euro milioni 93.9.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: