KLABU ya Chelsea imemteua kocha wa zamani wa Liverpoool Rafael Benitez kuiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu huu.
Uteuzi wa Benitez unakuja siku koja tu baada ya kufutwa kazi
kwa Roberto Di Matteo kutokana na matokeo mabaya katika mchuano wa
kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya baadaya kufungwa na Juventus
mabao 3 kwa 0.
Benitez mwenye umri wa miaka 52 anakuwa kocha wa tisa wa the Blues
chini ya uongozi wake Abramovich alipoanza kuogoza timu hiyo kuanzia
mwaka 2003.
Duru zinasema kuwa mmiliki wa klabu hii Roman Abramovich huenda
akamwajiri kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola msimu ujao.
Beniteza anatarjiwa kukutana na wachezaji wa chelsea hivi leo na
kuanza mazoezi kabla ya kucheza na Manchester City mwishoni mwa juma

0 comments:
Post a Comment