BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAHAKAMA YA ICC YAAGIZA KUKAMATWA MARA MOJA KWA BOSCO NTAGANDA.

Mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda 
Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda.


 Muendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC Fatou Bensouda amesema jenerali muasi nchini Jamuhuri ya kikdemorasia ya Congo Jean Bosco Ntaganda na kiongozi mkuu wa kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda waliopiga kambi nchini Congo, Sylvestre Rudacumura wanaotafutwa na mahakama hiyo, wanatakiwa wakamatwe mara moja.

Mwanamama huyo amesema kuwa muda wote viongozi hao watakuwa huru hali ya usalama itasalia kuwa mbaya katika eneo zima la ukanda wa maziwa makuu na sasa wamekuwa kitisho kikuu kwa wananchi wa maeneo hayo.

Jenerali wa zamani wa jeshi la Congo ambae anashukiwa kuwa kiongozi wa waasi wa kundi la M23 lililoundwa Mei mwaka huu, Jean Bosco Ntaganda anatafutwa na mahakama ya ICC kwa makosa ya kivita na mauaji ya kivita yaliofanyika mwaka 2002 na 2003 Jimboni Ituri. Kwa mujibu wa Ofisi ya Mahakama, Ntaganda amekuwa kichocheo katika machafuko ya huko Kivu.

Naye kamanda mkuu wa waasi wa kundi la FDLR Sylvestre Mudacumura anaechukuliwa kuwa kiongozi mkuu wa vurugu katika ukanda wa maziwa makuu anatafutwa na mahakama ya ICC kwa makosa ya kivita yaliyotekelezwa mwaka 2009 na 2010 katika mkoa wa Kivu nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: