BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUMBE TANZANIA KUNA WANAUME VIKOJOZI LAKI TANO KULIKO KENYE NA UGANDA ?.

 
Mmoja wa vikojozi akiwa amejikojolea akiwa usingizini.
 
TANZANIA ina idadi kubwa zaidi ya watu wazima wanaokojoa vitandani kuliko kenya na hata Uganda.

Tanzania ina watu wazima vikojozi, laki 5 wakati Kenya inafuata kwa ukaribu kabisa kwa kuwa na vikojozi wanaume na wanawake laki laki 4 tu huku Uganda ikishika mkia ikiwa na vikojozi chini ya idadi hiyo hapo.

Wanasayansi wanasema tatizo hilo la watu wazima kukojoa ni kubwa na linasumbua wengi lakini kwa sababu ni jambo la aibu wengi hawataki kulijadili.

Kuna mameneja, wabunge na hata mawaziri ambao ni vikojozi
Takwimu zinasema kwamba katika kila watu wazima 100, mmoja wao ni kikojozi.

hivyo nchini ikiwa na idadi kubwa ya watu milioni 50 kama Tanzania, basi jua kuwa watu wazima laki 5, yaani watu nusu milioni wanakojoa wakiwa usingizini hata kama wana wapenzi wao ama wake zao.

Jee unajua kuwa nchini uingereza kuna chama cha vikojozi ?.

 Watu wazima wanaokojoa wakiwa usingizini mjini London wameanzisha chama kinachoitwa The Bladder And Bowel Foundation.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: