BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Museveni na Kagame hawatokubali kupinduliwa kwa serikali na kundi lolote.

 
M23 rebels assemble police in Goma.
 
 VIONGOZI wa Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sauti moja wamelitaka kundi la waasi la M23 lililouteka mji wa Goma siku ya Jumatatu usiku, kuondoka nmjini humo na hawatokubali mapinduzi dhidi ya serikali yeyote ya kanda ya maziwa makuu.

Rais Museveni wa Uganda akiuliza watafanya nini ikiwa kundi litakata kuondoka alisema "wataona chamtema kuni".

Marais Yoweri Museveni, Paul Kagame na Joseph Kabila walizungumza na waandishi habari baada ya mazungumzo yao na kueleza kwamba ingawa wapiganaji wa M23 wanamadai yaliyo ya haki lakini hawawezi kutumia nguvu kupindua serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Rais Kabila amesema yuko tayari kuyasikiliza malalamiko ya waasi na atafanya kila awezalo kuyashughulikia.

Kwa Upande wake rais Kagame amesema kuhudhuria kwake mazungumzo hayo kunamaanisha anataka amani kwa kanda nzima, bila ya kutilia maanani sula la waandishi habari ikiwa anawaunga mkono wapiganaji wa M23.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: