
BAADA ya mapigano ya siku nane Israel na wapiganaji wa Hamas
wamekubaliana kuziweka silaha chini.
Pande mbili hizo ziliyasimamisha
mapigano kuanzia saa moja ya usiku hapo jana makubaliano hayo yalifikiwa kwa upatinishi wa Misri.
Hatua hiyo
ilitangazwa mjini Cairo na Waziri wa mambo ya nje wa Misri Kamel Amr
kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo Waziri wa mambo ya nje wa
Marekani Hillary Clinton pia alikuwapo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepongeza hatua hiyo ya
kusimamisha mapigano.
Katika tamko lake Baraza hilo la wanachama 15
limesema limesikitishwa juu ya vifo vya watu na limetoa mwito wa
kuhakikisha usalama wa raia na kuwalinda kwa mujibu wa sheria za
kimataifa.
Baraza hilo pia limezitaka pande mbili za mgogoro ziitekeleze hatua hiyo
ya kusimamisha mapigano. Limepongeza juhudi za Rais wa Misri Mohamed
Mursi katika kuleta amani.
Pia limempongeza Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-moon kwa juhudi zake wakati wa ziara yake katika
Mashariki ya Kati
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Ehud Barak.
Mapatano hayo yamekomesha siku nane za mauaji kwenye Ukanda wa Gaza
na kusini mwa Israel.
Wapalestina zaidi ya 150 na Waisraeli watano
waliuawa. Miundo mbinu kadhaa pia iliteketezwa.
Wapiganaji wa Hamas
waliishambulia Israel kwa mamia ya roketi hadi mji wa Tel-Aviv na
majeshi ya Israel yaliushambulia Ukanda wa Gaza kwa ndege.
Kiongozi wa Hamas Khaled Meshaal ameiunga mkono hatua ya kusimamisha
mapigano na ameielezea kuwa ni kushindwa kwa Israel.
Kwa upande wake
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amekubali kutoa fursa
ya kuleta amani, lakini wakati huo huo ameonya kwamba atakuwa tayari
kuchukua hatua kali za kijeshi ikiwa itakuwa lazima.
Muda mfupi kabla ya
kufikiwa mapatano ya kusimamisha vita, majeshi ya Israel na wapiganaji
wa Hamas waliendelea kushambuliana.
Hapo jana bomu liliripuka ndani ya basi katika mji wa Tel-Aviv.
Risasi na fataki zilifyatuliwa hewani katika mji wote wa Gaza City
huku mamia kwa mamia ya watu wakijitokeza barabarani kusherehekea.

0 comments:
Post a Comment