MKUTANO wa 18 wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi umefunguliwa
mjini Doha, bila ya kuwepo matumaini ya kufikiwa makubaliano ya
kupunguza moshi wa viwandani.
Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni namna ya kufikiwa itifaki ya pili
ya Kyoto ,kubuni njia ya kupatikana makubaliano jumla hadi ifikapo mwaka
2015 na kupatiwa misaada ya fedha nchi zinazokabiliwa na hatari zaidi
ya kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi.
Wataalam wanahofia ikiwa hatua hazitachukuliwa janga la joto mfano wa
lile lililoshuhudiwa Urusi msimu wa kiangazi mwaka 2010 linaweza kuzuka
upya, na kima cha maji ya bahari kikapanda huku mataifa yanayoinukia
yakikabiliwa na balaa lisilo na mfano la ukame.
"Bila ya kuwajibika na kuchukua hatua zinazohitajika kupunguza moshi
unaotoka viwandani, hali ya ujoto itaongezeka kwa nyuzi joto tatu
ulimwenguni,ikilinganishwa na hali namna ilivyokuwa kabla ya enzi za
viwanda.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyokabidhiwa benki kuu ya dunia
na taasisi ya utafiti wa mabadiliko ya tabia nchi ya mjini Postdam
nchini Ujerumani.
Ukame nchini India.
Hata hivyo hakuna anaetegemea kama mkutano huu wa Doha utakaoendelea
hadi December 7 ijayo,utapitisha hatua zozote za maana kusaidia
kupunguza moshi wa viwandani.
Sababu ya hayo anasema Sven Harmeling wa
shirika la ulinzi wa mazingira linaloshughulikia sera za mabadiliko ya
tabia nchi ulimwenguni.
"ni ile hali kwamba mengi yameshatangazwa katika
mikutano iliopita na nchi nyingi kurekebisha sheria zao, kwa hivyo
itakuwa shida kusema kama nchi hizo zitatoa ahadi yoyote ikiwa hazina
hakika kama malengo yaliyowekwa hadi sasa yatafikiwa."
Baadhi ya mataifa yanayoinukia yanategemea kupatiwa ahadi anaendelea
kusema Sven Harmeling:
"Kuna zaidi ya nchi 100 ambazo bado hazijatamka
lolote kuhusu hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi,miongoni
mwa nchi hizo,zinakutikana pia Philippines,Thailand,na pia nchi za
kiarabu,mfano Saud Arabia na Qatar.
Joto linasababisha milima ya theluji kuyayuka Greenland.
Ufanisi au kushindwqa mkutano wa Doha kutategemea kama maridhiano
yatafikiwa ya kurefusha itifaki ya Kyoto.
Nchi za Umoja wa Ulaya zinataka
muda wa itifaki hiyo ambao utamalizika mwishoni mwa mwaka huu,urefushwe
hadi mwishoni mwa mwaka 2020 ambapo mataifa yanayoinukia yatawajibika
nayo pia kupunguza moshi wa viwandani.Lakini wawakilishi wa mataifa
mengine,wanapendelea itifaki ya Kyoto irefushwe kwa miaka mitano badala
ya minane.
0 comments:
Post a Comment