MSANII HUSSEIN MKIETY a.k.a SHARO MILIONEA ENZI ZA UHAI WAKE.
Msanii wa muziki, maigizo na vichekesho wa nchini Tanzania Hussein Ramadhani (27) maarufu kama Sharo Milionea anatarajiwa kuzikwa kesho mkoani Tanga.
Sharo Milionea amefariki dunia jana jumatatu majira ya saa
mbili usiku baada ya gari alilokuwa anaendesha lenye namba za usajili
T478 BVR Toyota Harrier kupinduka mara tatu na kusababisha kifo chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Prudence Massawe alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa Msanii huyo alikumbwa na ajali hiyo katika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza mkoani Tanga wakati akitokea jijini Dar es salaam.
Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini alinusurika katika ajali nyingine ya basi la Taqwa alilokuwa akisafiria kutoka nchi ya Burundi baada ya basi hilo kupata ajali na kupinduka eneo la Mikese mkoani Morogoro wakati akirejea jijini Dar es salaam Januari 5 mwaka huu.
Kifo cha Sharo Milionea kimeibua simanzi na vilio kwa wapenzi wa msanii huyo wakati bado tasnia ya filamu ikiwa katika maombolezo ya kifo cha msanii John Steven aliyefariki dunia novemba 24 na anatarajiwa kuzikwa kesho jumatano jijini Dar es salaam.

Kufuatia kifo hicho cha msanii huyo, msaani mwenzake King Majuto akikimbizwa Hospitali baada ya kushikwa na presha, hivyo kutishia hali ya afya yake.
Mtoto wa King Majuto, Hamza Majuto,
alieleza kuwa hali ya baba yake inaendelea vizuri
kutokana na kuumizwa zaidi na msiba wa Sharomlionea anayetamba katika
ulingo wa filamu na muziki hapa nchini.

0 comments:
Post a Comment