KUMETOKEA ghasia kadha kaskazini mwa Nigeria katika eneo la mbali kaskazini-mashariki mwa nchi, watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko
Haram, walishambulia kanisa, kituo cha polisi, na ofisi za uhamiaji na ushuru katika mji wa Gamboru-Ngala, karibu na mpaka wa Cameroon.
Askari polisi wawili waliuwawa.
Pia kumetokea mapambano baina ya watu waliokuwa na silaha na askari wa usalama kwenye mji wa Azare, katika jimbo la Bauchi, kaskazini mashariki mwa nchi.
Wakaazi wa huko wanasema washambuliaji wawili waliuwawa na wa tatu amejificha ndani ya nyumba ambayo sasa imezingirwa na polisi.
0 comments:
Post a Comment