RAIS wa Wapalestina, Mahmoud Abbas, aliwaambia wafuasi
maelfu katika Ufukwe wa Magharibi "tuna taifa sasa".
Amekaribishwa kama shujaa baada ya kufanya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupiga kura kupandisha hadhi ya Wapalestina.
Akiwahutubia wafuasi wake mjini Ramallah, Ufukwe wa Magharibi, Rais Abbas alisema njia ilikuwa ndefu na shinikizo nyingi sana, lakini Wapalestina walisimama kidete na kushinda.
"Tulikwenda New York, tumebeba ujumbe wa uchungu na ndoto ya watu wetu kukabidhi kwa ulimwengu ujumbe wa haki na uhuru.
Ulimwengu umetoa kauli kwa sauti kubwa na kusema kuwa.
ndio liwepo taifa la Palestina.
Haki za Wapalestina, ndio.
Uhuru wa Palestina, naam.
Uhasama, la.
Makaazi ya walowezi, hapana.
Kuikalia Palestina, sivyo".
0 comments:
Post a Comment