Wananchi wa Syria wakiangalia magari yaliolipuliwa na
mabomu.
MILIPUKO ya mabomu iliyotokea kwa wakati mmoja katika kitongoji cha mji mkuu wa Syria Damascus imeuwa watu wapatao 34.
Televisheni ya taifa ya Syria ilionyesha picha za eneo la tukio eneo lenye wakristo wengi na waumini wa dhehebu la Druze . Magari yaliyogonganishwa na milipuko hiyo na mabaki ya majengo yalichafua mitaa.
Wanaharakati wanasema kuna ishara kwamba kulikuwa na milipuko mingine midogo miwili zaidi ingawa haikuwa wazi kama mtu yeyote alijeruhiwa.
Shirika la habari la SANA linasema shambulizi hilo la leo ni kazi ya ugaidi , neno ambalo serikali ya Syria inatumia dhidi ya majeshi ya wapinzani na waasi. Hii ni mara ya pili eneo hili limelengwa katika miezi kadhaa iliyopita.
0 comments:
Post a Comment