BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM MORO YAFANYA TATHININI YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA HICHO KUANZIA MWAKA 2010/2015 KATIKA MKUTANO WA HADHARA UWANJA WA SHUJAA.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris kulia akionyesha moja kadi ya Chadema mara baada ya Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Morogoro kuhamia CCM wakati wa mkutano wa hadhara wa kutathimini ilani ya CCM kwa mwaka 2012/2015 uliofanyika kwenye uwanja wa Shujaa kata ya Mjipya mkoani hapa. 
 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris akizungumza jambo wakati wa mkutano huo wa hadhara wa kutathimini ilani ya CCM kwa mwaka 2012/2015. 
Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalam mkoa wa Morogoro pia mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera naye akihutumia mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akiteta jambo na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris katika mkutano huo. 
 Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood ambaye pia ni Mjumbe wa NEC wilaya ya Morooro naye akizungumza katika mkutano huo ambapo ulitoa fursa ya viongozi kueleza majukumu mbalimbali waliyofanya ndani ya chama hicho.  

Abel Luanda aliyekuwa Katibu wa chadema mkoa wa Morogoro kushoto na wanachama wengine wa vyma vya upinzani akizungumza jambo mara baada ya kurejesha kadi za vyama vyao ikiwemo Chadema kwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris kulia.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Juma Nondo akielezea jambo umati uliohudhuria mkutano huo kazi zilizofanywa na Halmashauri chini ya usimamizi wake akishirikia na baraza la madiwani.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Mhe, Kalogeris akiteta jambo na Katibu wa CCM mkoa, Sixtus Mapunda katikati na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joelb Bendera kulia wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Morogoro Fikiri Juma kulia akiwaeleza jambo wabunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdulllaziz Abood kushoto na Dkt Lucy Nkya katikati wa jimbo la Morogoro kushini mashariki wakati wa mkutano huo.


 Sehemu ya wananchama wa chama hicho cha CCM wakifuatilia matuki ya mkutano huo.
 Mpiga Picha za kituo cha Luninga cha Abood Media Athman Shikiondo akiwajibika kwa kuchukua picha katika matukio yaliyokuwa yakiendelea.


MWENYEKITI mpya wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris ametoa onyo kali kwa kutoa mwezi mmoja kwa viongozi watatu ndani ya chama hicho kutafuta ufumbuzi wa kudumu kuhusu kuwatafutia eneo wafanyabiashara wadogodogo maarufu kama (Wamachinga) ili waweze kufanya biashara na kuondokana adha wanayopata ya kufanya biashara katika maeneo ambayo hayarusiwa mkoani hapa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho wa kutathimini ilani ya chama hicho kwa viongozi walioingia madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010/2015 katika uwanja wa Shujaa mkoani hapa jana, Kalogeris alisema kuwa ipo haja ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya wafanyabiashara hao kutafitiwa maeneo ya kufanyabiashara.

Kalogeris alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo analazimika kuteua viongozi watatu wa juu wa chama hicho ili kuweza kulitafutia ufumbuzi tatizo la wamachinga la kufanya biasha katika maeneo yasiyoruhusiwa ndani ya Manispaa hiyo.

Aliwataja viongozi hao ambao amewateua kushulikia suala hilo kuwa ni mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood, Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Morogoro, Fikiri Juma ambao watakuwa na jukumu la kutafuta eneo la wafanyabiashara kufanya biashara na kuwa ametoa mwezi mmoja ili kupata ufumbuzi huo wa tatizo hilo.

“Hawa wafanyabiashara ni wapigakura wetu na moja ya sera za CCM ni kuwawezesha kila mwananchi anajikwamua kiuchumi katika ngazi mbalimbali ikiwemo na mtu mmoja mmoja hivyo hawa wachinga wanapaswa kutafutiwa eneo maalumu ambalo watafanya biashara zao bila kuwa na bughuza” alisema Kalogeris.

Aidha Kalogeris alisema kuwa endapo viongozi hao watashindwa kutatua kero hiyo basi kamati ya maadili ya chama chicho itachukua hatua kali dhidi yao kwani lengo kuu ni kuona mji wa Morogoro unakuwa katika hali ya usafi lakini pia wafanyabiashara wanapatiwa maeneo ambayo halmashauri itaweza kukusanya ushuru tofauti na hivi ambao ushuru huo wana ukosa kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Mwenyekiti huyu ambaye ni mbunge wa jimbo la Morogoro kusini alisema kuwa moja ya faida kubwa ya kuwatafutia wafanyabiashara hao wa biashara ndogo ndogo itasaidia Manispaa kupunguza uchafu unaozagaa kila kona ya mji ambapo uchafu huo unaotokana na masalia ya uchafu wa wafabiasha hao.

Katika hatua nyingine viongozi wawili mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Abdullaziz Abood na Meya wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo walikuwa vivutio vikubwa wa wananchama wa chama hicho na wananchi wengine waliohudhuria mkutano huo hasa kwa kila mmoja namna avyojigamba kwa kutekeleza ilani ya chama hivyo kwa asilimia kubwa mara baada ya kushika madaraka yao.

Majigambo hayo yalianzia kwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kueleza kazi zilizofanywa na halmashauri ikishirikiana bega kwa bega na baraza la madiwa kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami tangu mwaka 2010 hadi 2012 kwa kuvuka malengo waliyojiwekea ya kujenga barabara kutoka kilometa mbili kwa mwaka hadi kilometa tisa ndani ya mitaa ya Manispaa mjini na kutangaza mikakati ya ujenzi wa barabara nyingine na kuwa kasi hiyo itawafanya wakazi wake kupata maendeleo kwa haraka.

Naye mbunge wa jimbo la Morogoro mjini alijinadi katika mkutano huo kuwa moja ya utekelezaji wa ilani hiyo akiwa mbunge ameweza kuwawesha vikundi vidogo vidogo vya akinamama zaidi 40 huku akitumia mabilioni ya fedha kwa kuwapatia mtaji ambao wanakopesha ili kila mwanakikundi kuweza kujikwamua na hali ngumu ya uchumi.

Abood ambaye pia ni  Mjumbe wa NEC Wilaya ya Morogoro mjini ametoa ahadi ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa kuwaondoa kero ya wanafunzi kupata usumbufu wakati wakipanda daladala kwenda na kurudi shule kwa kununua mabasi ambayo yatatoa huduma ya usafi kwa wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari ndani ya Manispaa hiyo huku wapambe wao wakiwapongeza viongozi hao kwa kuwasgangilia na kuibua shangwe na vifijo dhidi yao.

Mkutano huo ambao uliwawezesha viongozi ndani ya chama hicho kueleza utendaji wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya kata na mkoa huku viongozi wa ngazi za juu za chama hicho wakipata fursa ya kueleza utekelezaji wao akiwemo mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Mbunge wa jimbo la Morogoro, Abdullaziz Abood, Meya Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo, Mjumbe wa NEC Wilaya ya Mvomero, Sadik Suleiman Murad.

Wengine ni mbunge wa jimbo la Morogoro kusini mashariki, Dkt Lucy Nkya ambaye naye alieleza sera utekelezaji wa sera hiyo kwa kuunga mkono CCM kwa kuwaptia huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kata ya Chamwino Manispaa ya Morogoro ikiwezo na kuwasomesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu zaidi ya wanafunzi zaidi 30 kwa mwaka kupitia shirika la Faraja Trast Fund.

Hatua hiyo ya Mwenyekiti wa CCM mkoa huo imekuja baada ya kuwezo kwa malumbano ya hoja juu ya wafanyabiashara hao huku Meya wa Manispaa ya Morogoro na Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini ambaye amekuwa akipinga vikali hoja ya kupinga kuondolewa kwa wafanyabiashara katikati ya mji huo kwa madai kuwa halmashauri inapaswa kuwafutia kwanza eneo la kufanyia biashara zao.

Wakati Meya wa Manispaa hiyo akisimamia sheria za kuwaondoa wafanyabiasha hao kuondoka katikati ya mji na kudai kuwa ndicho chanzo kimojawapo cha mji huo kuwa mchafu kutokana na kuacha uchafu ukizagaa sehemu mbalimbali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: