RAIS Mursi wa Misri ameitisha kura ya maoni Desemba 15 kuhusiana na katiba mpya, kwa matumaini ya kumaliza maandamano baada ya tamko lake la kujilimbikizia madaraka,wakati waungaji wake mkono wakiandamana mjini Cairo.
Uidhinishaji wa katiba hiyo iliyotayarishwa na baraza ambalo linadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na washirika wake wa makundi ya Kiislamu, utaondoa amri iliyotolewa Novemba 22 ambayo kwa muda inamkinga Mursi dhidi ya uchunguzi wa mahakama na kuzusha matamshi ya kuonyesha wasi wasi kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Amri hiyo iliitumbukiza nchi hiyo katika mzozo wake mbaya kabisa kuwahi kutokea tangu pale Mursi aliposhinda katika uchaguzi mwezi Juni na kuzusha maandamano nchi nzima pamoja na ghasia ambamo watu wawili walipoteza maisha na mamia wamejeruhiwa.
Waungaji mkono rais Mursi wakiandamana mjini Cairo
Uchumi waathirika
Hali hiyo imeathiri uchumi ambao ulikuwa unaonesha dalili za kufufuka.
"Narudia wito wangu wa kuanzisha majadaliano muhimu ya kitaifa kuhusiana na wasi wasi uliopo katika taifa , kwa moyo mkunjufu kabisa na bila kuelemea upande wowote," amesema Mursi baada ya kupokea mswada wa mwisho kutoka katika baraza la kutunga katiba. " Tunapaswa kusonga mbele na kuacha nyuma kipindi cha mivutano na kutofautiana, na kuanza kazi ya ujunzi wa taifa."
Katiba ina lengo la kuwa sehemu muhimu ya kuelekea katika demokrasia ya kweli baada ya miongo mitatu ya utawala wa kiimla uliokuwa ukiungwa mkono na jeshi chini ya uongozi wa rais Hosni Mubarak.
Hata hivyo utungaji wa katiba hiyo umeleta mgawanyiko, na kuweka wazi mipasuko kati ya makundi ya Kiislamu ambayo hivi sasa yanashikilia madaraka na wapinzani wao.
Waandamanaji wakiwa katika uwanja wa Tahrir
Katiba ina mapungufu.
Maandamano katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo, eneo ambalo limekuwa kitovu cha maandamano dhidi ya Mubarak, wamekishutumu chama cha Mursi cha udugu wa Kiislamu katika kujaribu kulazimisha kuwa na katiba ambayo inamapungufu.
Mohammed El-Baradei
Viongozi wakuu wa upinzani kama Mohammed El Baradei amesema katika tovuti ya kijamii ya twita kuwa " Mapambano yataendelea " licha ya kura ya maoni na kwamba mswada wa katiba " unakandamiza haki za msingi za uhuru."
Viongozi wenye msimamo wa wastani ambao ni pamoja na katibu mkuu wa zamani wa jumuiya ya mataifa ya Kiarabu , Arab League, Amr Moussa, wamejitoa kutoka katika baraza hilo la kutunga katiba mwezi uliopita, kama walivyofanya wawakilishi wa Wakristo wachache nchini Misri.
Katibu mkuu wa zamani wa Arab League Amr Moussa
Mswada huo wa katiba una lugha yenye mapungufu ya makundi ya Kiislamu ambayo wapinzani wanasema inaweza kutumiwa kudhoofisha ukosoaji dhidi ya kuendewa kinyume haki za binadamu.
0 comments:
Post a Comment