MAWASILIANO ya internet nchini Syria yamerudi, baada ya simu kukatwa kwa
siku tatu mfululizo huku mapigano makali yakiendelea mjini Damascus.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema wakaazi wakati wote wanaishi na ghasia za mizinga na ndege za kivita zikiruka juu ya mji.
Habari za karibuni kabisa zaeleza kuwa mawasiliano ya mtandao wa internet sasa yanapatikana.
Mapigano makali hasa yanaendelea katika sehemu za kusini na mashariki mwa mji mkuu.
0 comments:
Post a Comment