Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi.
KATIKA kukabiliana na janga la vifo vya watoto na wanawake wakati wa kujifungua, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na nchi ya Australia, jana zimezindua programu ya mafunzo kwa wakunga na wauguzi itakayogharimu Sh2.4 bilioni.
Programu hiyo ya miaka miwili ambayo itafanyika katika Hospitali tatu za hapa nchini, imeambatana na msaada wa magari mawili ya kubebeba wagonjwa aina ya Landcruiser yenye thamani ya Sh240 milioni.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli, katika programu hiyo mafunzo kwa wauguzi yatatolewa katika Hospitali na Zahanati katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Kikuli alisema mafunzo hayo yatatolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Amana na Mikocheni jijini Dar es Salaam, sambamba na Kituo cha Afya cha Masaki na Zahanati ya Masanganya wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli, katika programu hiyo mafunzo kwa wauguzi yatatolewa katika Hospitali na Zahanati katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Kikuli alisema mafunzo hayo yatatolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Amana na Mikocheni jijini Dar es Salaam, sambamba na Kituo cha Afya cha Masaki na Zahanati ya Masanganya wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Programu hiyo ambayo inaratibiwa na Mtandao wa Ushirikiano wa Watoa Huduma za Afya na Waelimishaji kutoka Australia Magharibi (Ghawa), ilianza kwa kukarabati madarasa ya Shule ya Wakunga iliyopo Muhimbili ikiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa taaluma hiyo.
Kaimu Katibu Mkuu alisema, Tanzania bado ina kiwango cha juu cha wanawake wanofariki wakati wakijifungua, ambapo wanawake 454 kati ya laki moja hupoteza maisha.
Kikuli alisema kuwa Wizara yake inataka kupunguza idadi hiyo hadi kufikia 68 katika elfu moja, na programu hiyo ni moja ya mikakati ya kufikia lengo hilo.
“Serikali imejitahidi sana kupunguza idadi hiyo, lakini peke yake haiwezi kufanya kila kitu inahitaji wadau na asasi zisizo za kiserikali katika kutatua changamoto hii,” alisema Kikuli.
Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema Programu hiyo itajenga uwezo kwa wauguzi na kusaidia kupunguza vifo vya kinamama na watoto.
“Tumeweka kipaumbele katika kushughulikia tatizo hili la vifo vya watoto, lakini pia tunatazama ni njia zipi bora zitakazosaidia kinamama kujifungua salama,” alisema.
Kiongozi huyo alifafanua kuwa asilimia 90 ya wajawazito wanaohudhuria kliniki ni asilimia 50 ndiyo wanajifungua katika mazingira salama.
“Hatua hii itakuwa ni motisha kwao kuja kujifungulia katika vituo vya afya,” alisema Kikuli.
Akizungumzia msaada wa magari ya kubebea wagonjwa ambayo yatatumika wilayani Kisarawe. Kikuli alisema kwa kiasi kikubwa usafiri huo utapunguza tatizo wilayani humo hasa kwa wakina mama wajawazito.
0 comments:
Post a Comment