Walowezi wa kiyahudi wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi.
Israeli inasema inapanga kuongeza nyumba elfu tatu kwa makaazi yaliopo tayari na inatarajia kuongeza makaazi mapya kuunganisha yale yaliopo katika ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki.
Ilitangaza mpango huo kufuatia kura iliyopigwa katika Umoja wa mataifa iliyoipandisha Palestina hadhi kuwa dola muangalizi katika umoja huo.
Hapo jana kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas alipokewa kwa shangwe mjini Ramallah katika ukingo wa Magharibi aliporudi nyumbani kutoka kwenye mkutano huo.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameahidi kuendelea na mpango wake wa ujenzi.
Katika taarifa yake Jumapili, Bwana Ban alielezea wasiwasi mkubwa kuhusu mpango ulioidhinishwa wa nyumba mpya elfu tatu zinazotarajiwa kujengwa Mashariki mwa Jerusalem na katika ukingo wa Magharibi.
Lakini alisisitiza kuwa mpango wowote wa kujenga makaazi katika sehemu inayojulikana kama E1, kati ya Jerusalem na makaazi yaliyoko Ukingo wa Magharibi ya Maaleh Adumim, lazima usitishwe.
"Hatua hii itakuwa pigo kubwa kwa fursa iliyopo ya mazungumzo ya amani'' alisema bwana Ban.
Marekani ilisema kuwa mpango huo hausaidii chochote bali utaathiri hatua zilizofikiwa za amani.
Naye Mkuu wa sera katika Muungano wa Ulaya Catherene Ashton, alielezea wasiwasi kuhusu mpango wa ujenzi wa makaazi mengine ya walowezi.
0 comments:
Post a Comment