BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC KUWEKA REKODI NYINGINE KWA LIBOLO FC ?.

Kwa ufupi:
Pambano la Azam linafanyika kwenye mji wa Juba, ambapo wanahitahi sare aina yoyote ili kusonga mbele raundi ya pili, Katika pambano la Simbalitakalochezwa saa tisa za Angola ikiwa ni saa 11 kwa saa za Afrika Mashariki na kati, Simba wataingia katika uwanja wa Calulukuumana na Libolo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 wiki mbili zilizopita muuaji akiwa Joao Martins.
 
Mrisho ngasa wa timu ya Simba akijaribu kumtoka beki wa Libolo ya Angola katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam. 
 
SIMBA leo wanakabiliwa na mtihani wa kufanya maajabu mengine katika historia ya soka Tanzania wakati watakapowavaa Recreativo Libolo ya Angola ugenini, huku Azam FC wakishuka dimbani kulinda ushindi wao wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Al Nasri ya Sudan Kusini.

Pambano la Azam linafanyika kwenye mji wa Juba, ambapo wanahitahi sare aina yoyote ili kusonga mbele raundi ya pili
Katika pambano la Simbalitakalochezwa saa tisa za Angola ikiwa ni saa 11 kwa saa za Afrika Mashariki na kati, Simba wataingia katika uwanja wa Calulukuumana na Libolo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 wiki mbili zilizopita muuaji akiwa Joao Martins.


Katika pambano la leo, kocha Patrick Liewing huenda akamkosa kiungo mahiri, Mwinyi Kazimoto ambaye tangu awasili nchini Angola amekuwa akisumbuliwa na jino.

Nafasi yake inatazamiwa kuchezwa na kinda, Abdallaa Seseme ambaye alikuwa nyota wa mchezo katika pambano la Ligi kuu dhidi ya Prisons wiki moja iliyopita. Kama Kazimoto akipata nafuu kabla ya mechi basi huenda Seseme akaanzia benchi.

Kocha Liewig ambaye ni raia wa Ufaransa amepanga kucheza soka la kushambulia na kutengeneza nafasi kwa ajili ya kurudisha bao la Martins ambalo limeiweka Simba katika nafasi mbaya ya kusonga mbele.

Tutajaribu kufunga mabao ya mapema kwa ajili ya kurudisha bao lao. 

Najua wachezaji wangu wanaweza kufanya hivyo kwa sababu katika mechi ya kwanza tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukutumia, wao walitengeneza chache na walitumia,î alisema Liewing.

Liewig pia aliongeza kuwa kutokana na wachezaji wengi wa Libolo kuwa na nguvu, stamina atawataka wachezaji wake wajaribu kukaa na mpira kwa muda mwingi wakiepuka matumizi ya nguvu ya Libolo.

Pambano hilo linatazamiwa kuchezeshwa na Mwamuzi wa kati, Nhleko Simanga kutoka Swaziland , waamuzi wasaidizi ni Nkhabela Bhekisizwe na Mbingo Petros pamoja na mwamuzi msaidizi Fabuze Mbongiseni wote kutoka kutoka Swaziland pia. Kamisaa wa pambano hilo ni Mandla Mazibuko kutoka Afrika Kusini.

Mwamuzi Simanga anaweza kuwa na bahati nyingine kwa Simba leo kwa sababu ndiye aliyechezesha mechi kati ya Simba na Shandy ya Sudan, ambapo Simba walishinda 3-0 kwa mabao ya Emmanuel Okwi, Haruna Moshi na Patrick Mutesa Mafisango ambaye kwa sasa ni marehemu.

Endapo Simba itashinda leo itakuwa imerudia historia ya mwaka 1979 ambapo ilifungwa 4-0 nyumbani na Mufulira Wanderers, lakini ikashinda 5-0 ugenini jijini Lusaka. 

Katika pambano la leo, Simba ambayo imefikia katika Hotel ya Ritz inayomilikiwa na tajiri wa Libolo, Lui Compos inatazamiwa kuwakilishwa na Juma Kaseja, Said Nassor Chollo, Amir Maftah, Juma Nyosso, Komanbil Keita, Shomari Kapombe, Haruna Chanongo, Amri Kiemba, Abdala Seseme, Felix Sunzu, Mrisho Ngassa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: