BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA NAIBU WAZIRI WA UJENZI WAKATI WA UKAGUZI NA KUTEMBELEA MIRADI YA KITAIFA KATIKA MAANDALIZI YA UJENZI WA DARAJA LA MTO KILOMBERO MKOANI MOROGORO.

 Naibu waziri wa wizara ya ujenzi, Gerson Lwenge kulia akifafanua jambo kwa mhandisi mkuu, Lianf Yan Ping kutoka kampuni ya ujenzi ya China Railway 15 Bureau Group Corporation wakati naibu waziri huyo alipotembelea na kukagua mradi wa kitaifa wa ujenzi wa daraja mto Kilombero ambalo litaunganisha wakazi wa wilaya mbili za mkoa wa Morogoro za Ulanga, Kilombero pamoja na mkoa wa Ruvuma katika feri ya Ifakara mkoani Morogoro.
Hapa Naibu waziri Lwenge kulia akifafanuliwa jambo na mkurugenzi wa Lucky Construction Ltd, Ibrahim Kissoky juu ya ujenzi wa maegesho ya kivuko cha Mv Kilombero 1 kwa upande wa wilaya ya Kilombero.
 Mbunge wa viti maalum Chadema Suzan Kiwanga kulia akimweleza jambo naibu waziri katika ziara hiyo.
Naibu waziri akitelemka katika Mv Kilombero wakati kuelekea katika ukaguzi wa ujenzi wa darahi kwa upande wa wilaya ya Ulanga, mbele yake ni mbunge wa viti maalum Suzan Kiwanga.
 Naibu waziri wa wizara ya ujenzi, Gerson Lwenge mbele akiongozana na Mhandisi wa mradi wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro (Tanroad), Salehe Juma kushoto na Kaimu Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro (Tanroad), Moses Kiula (mwenye kaunda suti nyeusi) wakati naibu waziri huyo alipotembelea na kukagua mradi wa kitaifa wa ujenzi wa daraja la mto Kilombero ambalo  litaunganisha
 wakazi wa wilaya mbili za mkoa wa Morogoro za Ulanga, Kilombero pamoja na mkoa wa Ruvuma katika feri ya Ifakara mkoani Morogoro.
 Naibu Waziri akihutubia wananchi.
 Wananchi wakimsikiliza naibu waziri.

JUMA MTANDA, KILOMBERO.

ZAIDI ya sh 53.214 bilioni zinatarajia kutumika katika ujenzi wa darajajipya la mto Kilombero huku serikali ikitoa ovyo kwa mkandalasi kuhakikisha kuwa ujenzi wa daraja hilo unakamilika kwa wakati uliopangwa ili ifikapo januari 21 mwaka 2015 liwe limekamilika.
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kilombero na Ulanga katika kivuko cha mto Kilombero Ifakara Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge alisema kuwa serikali tayari imeingia mkataba wa ujenzi wa daraja hilo na mkandalazi wa China Railway 15 Bureau Group Corporation kwa thamani ya zaidi ya sh 53.214 bilioni.
Lwenge alisema kuwa mkandalasi tayari ameanza kuwa nyuma ya muda wa maandalizi na kuwa asitegemee kama serikali itaongeza muda ujenzi wa ujenzi wa daraja hilo kwani kufika januari 21 mwaka 2015 ili Rais Jakaya Kilwete kabla ya kuondoka madarakani aweze kukamilisha ahadi yake.
“Ujenzi wa daraja la mto Kilombero ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) ahadi ambayo Rais Jakaya Kikwete ameotoa ya kujengadaraja jipya katika mto Kilombero” alisema Lwenge.
Lwenge alisema kuwa daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 384, upana 7.5 na njia ya waenda kwa miguu na baiskeli upana wake ni 1.5, ujenzi wa makalavati makubwa 35,  makalavati madogo 18, na barabara za kuingia katika daraja hilo zenye jumla urefu wabkilometa 9.142 zitakazojengwa kwa kiwango cha lami.
Alitaja vipimo vingine vya daraja na barabara kuwa ni upana ni 6.5 pamoja na mabega yenye upana wa mita 1.5 kila upande na mitaro ya kuondoa maji ya mvua pamoja na kazi ya kuzuia mmomonyoko wa udongo pembezoni mwa barabara na kuta za madaraja.
Naye Mhandisi wa mradi wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro (Tanroad), Salehe Juma alisema kuwa mpaka sasa mkandalasi huyo tayari amelipwa malipo ya awali kiasi cha sh 7.982 bilioni.
Juma alisema kuwa kuna changamoto imejitokeza, kwani mpaka sasa bado hajapatikana mhandisi mshauri kwa ajili ya usimamizi wa mradi huo na kazi za usimamizi zinasimamiwa na ofisi ya mtendaji mkuu wa wakala wa barabara.
Hatua ya ujenzi iliyofikia kwa sasa ni mkandalasi kuendelea na maandalizi ya wataalamu, ujenzi wa kambi pamoja na kambi ya mhandisi mshauri na kuwa tayari amefikia asilimia 33 ya kazi ya maandalizi.
Naibu waziri huyo wa Ujenzi yupo katika ziara ya siku mbili katika mkoa wa Morogoro anatembelea miradi ya kitaifa pamoja na kukagua ujenzi wa miradi hiyo ikiwemo barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami katika wilaya ya Kilosa, Kilombero na Kilombero.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: