BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK KIKWETE, DK SHEIN WAWAONGOZA WAZANZABAR KATIKA HAFLA YA KISOMO CHA HITMA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisoma Hitma Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya CCm Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo kila ikifika siku kama hii wananchi kwa ujumla wao hukusanyika kuomba dua kama hii. 
Wake wa Viongozi Wakuu wakiwemo na viongozi wa taasisi za Kinamama wakinyanyua mikono juu kumuombea dua  Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.katika kaburi lake huko CCM Kisiwandui mjini Zanzibar,baada ya kisomo cha Hitma leo
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,(kulia) akiwa na Wake wa Viongozi mbali mbali katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCK Kisiwandui Mjini Zanzibar Leo.
Akina mama wa Kiislamu wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Viongozi wengine katika kisomo cha HItmaya Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: