BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KOROSHO ZINA FAIDA KUBWA KWA AKINAMAMA WAJAWAZITO, WATOTO. WAZIRI MALIMA.


Naibu waziri kilimo na Chakula Adam Malima, akizungumza baada ya kuzindua maadhimisho ya siku ya kutafuna korosho yaliyofanyika katika maonyesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mteja akinunua Korosho katika banda la maonyesho ya Saabasaba Dar es Saalaam wakati wa kilele cha siku ya kuonja korosho nchini Julai 05 mwaka huu.

Mfanyakazi wa bodi ya korosho , Juma Kimante akigawa korosho kuadhimisha siku ya kuonja korosho.

Na Mwandishi wetu,Tanpress.
WATANZANIA wameaswa kujenga utamaduni wa kupenda kula korosho kwani zinajenga  afya hususani  kwa  akinamama wajawazito  na watoto wadogo, ambao huwezeshwa katika makuzi bora.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Kilimo na Chakula, Malima wakati akizindua siku ya kuonja korosho kwenye banda la bodi ya korosho lililopo kwenye maonyesho ya sabasaba.
Waziri Malima  alisema kuwa Tanzania inasifika du niani kwa kulima korosho safi na bora lakini wananchi wake hawana utamaduni wa kula hizo kororosho bad
ala yake wanapendelea kula biskuti  jambo ambalo ni kinyume na nchi zingine.
“Watanzania hatupendi kulakorosho wakati  zinapatikana kwa  wingi hapa nchini ,nawaasa wazazi wajitahidi kila wanapoandaa chakula korosho iwe pembeni kwa sababu  ni nzuri hata kwa  watoto…..pia naiagiza bodi ya korosho kutengeneza vipindi vya kuhamasisha ulaji wa korosho vichezwe kwenye redio na televisheni”amesema Waziri Maalima.
Naye Katibu Mtendaji katika  mfuko wa kuendeleza korosho nchini (CIDTF) Suleman  Lenga amewashauri wakulima kutambua kuwa hapa nchini kuna soko kubwa la korosho badala  ya kutegemea soko la nje wanaweza kuuza hapa.
“kwa kutambua hilo mfuko wa  CIDTF umeambua kuwalipia gharama za kubangua korosho wakulima wadogo ili waweze kuziongeza thamani wakati wa kuuza hivyo wananchi wanapaswa kuanza kulakorosho kwa wingi ziweze kuletwa sokoni kwa wingi pia”amesema Lenga. 
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA MDAU, MOBINI SARYA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: