BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MCHAWI WA KIKE AMWAGIWA CHUMVI NCHINI ZIMBABWE.

MCHAWI AANGUKA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KULOGA, HUKO NCHINI ZIMBABWE.

MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Sabina Rokuzhe hivi karibuni alileta kizaazaa katika mji wa Dzivarase baada ya kupata ajali wakati akifanya shughuli zake za ushirikiana.
 
Kukumbwa kwa mkasa huo kwa mwanamke huyu ilimlazimu kuwapigia magoti wananchi waliotaka kumsurubu.
Rokuzhe alikuwa na aibu hiyo  ambapo alilazimika kuwaeleza ukweli wananchi hao kuwa yeye ni mchawi na amedondoka alipokuwa anaruka kwenye ungo akitokea kwenye safari zake ya kuloga huko Masvingo nchini Zimbabwe.

Alikutwa kwenye nyumba ya Mbuya Annah Kamupaundi, akaanza kuwaomba watu waliomzunguka wasimpige ,akasema pia katembelea nyumba kadhaa katika eneo hilo.

Mmoja wao aliyemuona asubuhi mapema ni Mrs Alice Hundi (37) ambae alisema aliamka baada ya kusikia mayowe ya mwanamke kwenye saa nane hivi usiku.

"Nilipomuona yuko uchi, nilimmwagia  chumvi usoni, akaanguka na kuanza kujizungusha zungusha chini. Tuliita polisi na akachukuliwa"

Polisi walitoa uhakika kwamba amechukuliwa na atapewa msaada wa psychiatric.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: