Mkuu
wa Mko wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akimkabidhi Ngao ya Jamii,
Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya mcheo wa
Ngao ya Jamii dhidi yao na Azam Fc, mchezo uliomalizika hivi punde
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mcheo huo Yanga
imeibuka na ushindi kiduchu kwa kuendeleza uteja kwa Azam Fc baada ya
kuifunga bao 1-0 lililofungwana Terela katika dakika 2 ya mcheo huo, bao
pekee lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo. PICHA KWA HISANI YA http://www.sufianimafoto.comBAO la Dakika ya Pili la Salum Telela leo limewakabidhi Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga,NGAO ya JAMII, walipoifunga Azam FC Bao 1-0 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuashiria kuanza kwa Msimu mpya wa Soka wa 2013/14.
NGAO YA JAMII-MABINGWA:
2001: Yanga 2 Simba 1
2009: Mtibwa Sugar 1 Yanga 0
2010: Yanga 0 Simba 0 (Penati 3-1)
2011: Simba 2 Yanga 0
2012: Simba 3 Azam 0
2013: Yanga 1 Azam 0
Licha ya kupata Bao la mapema kufuatia krosi ya Didier Kavumbagu kuunganishwa na Telela, Yanga pia waliathirika Dakika za mwanzo kwa kulazimika kubadilisha Wachezaji wao mara mbili kutokana na kuumia.
Katika Dakika ya 16, Yanga ilibidi wamuingize Mbuyu Twite kushika nafasi ya Kelvin Yondani alieumia na Dakika 8 baadae akaingizwa Kipa Deogratius Mun
ishi 'Dida' kuchukua nafasi majeruhi Ally Mustapha 'Barthez'.
Lakini dosari hiyo haikuwateteresha Yanga ambao walilinda Bao lao vizuri na kama wangekuwa makini wangeweza kupata Mabao mengine.
Moja ya nafasi safi ni ile frikiki ya Niyonzima katika Dakika ya 81 iliyogonga posti na kuokolewa.
Baada ya Mechi hii ya fungua pazia Msimu mpya, Ligi Kuu Vodacom, VPL, inatarajiwa kuanza Wikiendi ijayo hapo Jumamosi Agosti 24 ambapo Rtimu zote 14 zitakuwa dimbani na Mabingwa Yanga watakuwa Nyumbani kuanza na Timu iliyopanda Daraja Ashanti wakati Azam FC watakuwa huko Ugenini Manungu kucheza na Mtibwa Sugar.
VIKOSI:
YANGA: Ally Mustapha 'Barthez', Juma Abdul, David Luhende, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji', Saimon Msuva , Salum Telela, Jerson Tegete, Didier Kavumbagu, Haruna Niyonzima
Akiba: Deogratius Munishi 'Dida', Mbuyu Twite, Rajab Zahir, Frank Domayo, Nizar Khalfani, Said Bahanuzi, Hussein Javu.
AZAM FC:
Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco, Kipre Balou, Khamis Mcha.
Refa: Oden Mbaga.
LIGI KUU VODACOM:
RATIBA.
MECHI ZA UFUNGUZI:
Jumamosi Agosti 24
|
YANGA |
v |
ASHANTI UNITED |
UWANJA WA TAIFA |
DSM |
|
MTIBWA SUGAR |
v |
AZAM FC |
MANUNGU |
MOROGORO |
|
JKT OLJORO |
v |
COASTAL UNION |
SH. AMRI ABEID |
ARUSHA |
|
MGAMBO JKT |
v |
JKT RUVU |
MKWAKWANI |
TANGA |
|
RHINO RANGERS |
v |
SIMBA |
A.H. MWINYI |
TABORA |
|
MBEYA CITY |
v |
KAGERA SUGAR |
SOKOINE |
MBEYA |
|
RUVU SHOOTINGS |
v |
PRISONS |
MABATINI |
PWANI |

0 comments:
Post a Comment