BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AVEVA AWA URAIS MPYA WA KLABU YA SIMBA SC HUKU MICHAEL WAMBURA AKIENDELEA KUKUMBWA NA MIZENGWE.UCHAGUZI.


Rais mpya wa klabu ya Simba, Evans Aveva akihutubia katika katika mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam, jana. Picha na Michael Matemanga.
Dar es Salaam. 

Evans Aveva ameula baada ya kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa klabu ya Simba katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aveva alipata ushindi huo wa mithili ya kimbunga baada ya kupata kura 1845 na kumgaragaza mpinzani wake Andrew Tupa aliyepata kura 387 huku kura sita zikiharibika.


Katika nafasi ya Makamu wa Rais, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 1043 huku Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ akipata kura 413 na Swedy Mkwabi akipata kura 300.


Awali, aliyekuwa mgombea Urais wa klabu hiyo, Michael Wambura alizuiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kuingia kwenye Ukumbi.


Wambura, alienguliwa kwanza kwa kuwa amesimamishwa uanachama na baadaye kwa kukiuka taratibu za uchaguzi, alishindwa kupiga kura kutokana na uamuzi wa kumzuia kuingia ukumbini.


Kwa mujibu wa wasimamizi waliokuwa wakihakiki uhalali wa wanachama kwenye uchaguzi huo, jina la Wambura halikuwapo katika orodha ya wanachama wanaostahili kupiga kura.


Wambura kama walivyokuwa wanachama wengine, walifika katika eneo la uchaguzi kwa ajili ya kukamilisha haki hiyo ya kikatiba, lakini alionekana kushangazwa na uamuzi huo wa kuzuiwa kupiga kura.


Jibu alilopewa lilimfanya kuondoka maeneo hayo kwa hasira majira ya saa 4:00 asubuhi. Wakati hayo yakitokea, wafuasi wake walionekana kukasirishwa na kitendo hicho na kutaka kufanya fujo, hata hivyo askari waliokuwapo maeneo hayo walizima jitihada hizo.


Katika mkutano huo wa uchaguzi ulioanza rasmi saa 5:00 asubuhi, lilipomalizika zoezi la wagombea kujinadi, zoezi la kupiga kura liliibua vurugu nzito kutokana na wanachama wengine kukosa karatasi za kupigia kura kwa nafasi za rais na makamu wake.


Hali hiyo ilichangiwa na wanachama kushindwa kuwa na utulivu. Hata hivyo, baada ya muda zoezi hilo liliendelea kukiwa na utulivu mdogo katika zoezi hilo la kupiga kura lililoanza saa 9:00 alasiri na kura kuhesabiwa saa 11:00 jioni.MWANANCHI

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: